CEO INGWE: TULIENI AUSSEMS ANACOME

MASHABIKI kadhaa wa AFC Leopards wameanza kupandwa na presha baada ya  FKF kutangaza kurejea kwa msimu wa ligi kuu wiki ijayo.
Kinachowapa presha mashabiki hawa wa Ingwe ni hatma ya kocha wao Mbelgiji Patrick Aussems aliyeondoka nchini punde tu Rais Uhuru alipoweka lockdown.
Kocha huyo Mbelgiji alikwenda Ufaransa iliko familia yake.  Safari yake ilitafsiriwa na maelefu ya mashabiki wa Ingwe kwamba ndio jamaa kaaga na hatarudi. Hii ni kutokana na mtindo wa makocha wengi wa kigeni kuwa na tabia hiyo. Kila wanaporejea kwao kwa ajili ya likizo, wengi wao huwa hawarudi.
Na sasa baada ya FKF kutoa ratiba mpya, hofu hiyo imerudi tena mashabiki wakitaka kujua kama kweli jamaa anarudi ama  alishawatoka.
Hata hivyo Afisa Mkuu Mtendaji wa Ingwe, Victor Bwibo akichapa stori na safu hii, amesisitiza kuwa kocha huyo Mbelgiji wanamtarajia nchini katikati ya mwezi huu.
“Tunamtarajia arejee kabla ya katikati ya mwezi huu. Tunatumai alikuwa na muda wa kutosha kujienjoi na familia yake. Ameshapokea chanjo mbili za Covid-19 kule kwao na ni dhamira yetu kwamba yupo tayari kurejea kwa majukumu yake hivyo mashabiki wetu watulie na wala wasi hofu Aussems anacome” Bwibo kasema.
Vile vile Bwire kasema kuwa wameanza mazungumzo na straika wao matata Elvis Rupia kuhusu suala la kumrefushia mkataba nao.
Rupia ambaye ndio kinara wa magoli klabuni humo akiwa kucheka  na nyavu mara 11 kutokana na mechi 14, kasalia na miezi miwili tu kwenye mkataba wake wa sasa na Ingwe.
Alijiunga nao Januari mwaka huu akitokea Wazito FC kwa mkataba wa mkopo  wa miezi sita na huenda kocha Francis Kimanzi akamhitaji.
Wakati Rupia anauzwa kwa mkopo, Kimanzi hakuwa kateuliwa kocha wa Wazito. Kikosi cha Kimanzi kimekuwa kikifanya vizuri ingawaje kwenye upande wa  magoli wamekuwa wakilemewa na huenda kocha huyo akaamua kumrejesha Rupia nyumbani.