Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zola amvimbisha kichwa Hazard

Muktasari:

Kocha msaidizi wa Chelsea Gianfranco Zola ni kama amemvimbisha kichwa kiungo wa timu hiyo raia wa Ubelgiji, Eden Hazard, baada ya kusema iwapo ataamua kubaki na kumalizia soka lake hapo atakuwa ndiye mchezaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo.

London, England. Kocha msaidizi wa Chelsea, Gianfranco Zola, amesema kiungo Eden Hazard akifuta mpango wa kwenda Real Madrid na kukubali kubaki atakuwa nyota wa muda wote ndani ya klabu hiyo.

Hazard ambaye bado anashikilia mpango wa kutaka kuhama licha ya kuzuiwa kufanya hivyo kiangazi cha mwaka huu, alinukuliwa akisema siku moja atatimiza ndoto yake ya kutua Santiago Bernabeu.

Hata hivyo Zola amesema kwamba kutokana na kiwango anachokionyesha mchezaji huyo kutoka Ubelgiji ni wazi kuwa atajipatia heshima na thamani kubwa iwapo ataamua kumalizia soka lake Chelsea.

Mkataba wa sasa Hazard mwenye miaka 27 utamalizika Juni 2020 na klabu hiyo ilitaka kumuongezea mkataba mpya lakini amekataa akisema anasubiri hadi mkataba wa sasa umalizike.

Chelsea iliahidi kumpa mkataba mpya wa mshahara mnono ili kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya klabu hiyo ingawa Hazard mwenyewe ameonekana kutokuwa tayari kwa hilo.

Kwa sasa Zola ndiye anayeshikilia tunu hiyo ya mchezaji bora wa muda wote ndani ya Chelsea baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa klabu hiyo mwaka 2003.

Chini ya uongozi wa kocha Maurizio Sarri, Hazard ameendelea kuwa katika kiwango bora na laiti kama ataamua kuituliza akili yake kubaki Stamford Bridge, bila shaka hicho anachokisema Zola kitatimia

Kiungo huyo aliyetua Chelsea akitokea Lille ya Ufaransa mwaka 2012, amekuwa katika kiwango bora kinachomuingiza kikosi cha kwanza muda woteametwaa mataji mawili ya Ligi Kuu, moja la FA, Kombe la Ligi na Europa Ligi.

Msimu uliopita kiwango chake kilishuka kutokana na kutofautiana na kocha Antonio Conte, lakini msimu huu amerejea kwenye kiwango cha juu na tayari amefunga mabao kumi na kupika tisa katika michuano yote.

Mchezaji huyo ameshaitumikia Chelsea katika michezo 224 na amefunga mabao 77 katika michuano mbali mbali, amekuwa akifunga mabao ya kuamua matokeo katika mechi muhimu.

Mchezaji huyo anazitafuta rekodi zilizowekwa na nyota kadhaa waliotamba na kupata heshima kubwa ndani ya Chelsea katika miaka ya hivi karibuni akiwemo Didier Drogba aliyecheza mechi 244 na kufunga mabao 104, Frank Lampard, mechi 429 mabao 147 na John Terry mechi 492 mabao 41.

&&&&&