Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zizou achekelea ubingwa Sierra Leone

ZIZOU pict

Muktasari:

  • Kupunguzwa kwa pointi hizo kuliwapa nafasi Mogbwemo Queens kujihakikishia ubingwa bila kusubiri matokeo ya mechi zilizobaki.

BAADA ya Mogbwemo Queens inayoshiriki Ligi ya Wanawake Sierra Leone kutwaa ubingwa wa ligi mapema, kiungo Mbongo, Zuwena Aziz ‘Zizou’ amesema ilikuwa lazima wanyakue taji kutokana na mwendelezo mzuri waliokuwa nao. 

Mogbwemo Queens imebeba taji hilo ikiwa bado na mechi nne mkononi, hatua inayoonyesha ubora wao mkubwa msimu huu.

Ubingwa huo umeifanya timu hiyo kukata tiketi ya kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya WAFU A kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.

Akizungumza baada ya mafanikio hayo, Zizou amesema msimu huu umekuwa wa kipekee kwake, akifurahishwa na kiwango alichoonyesha katika ligi hiyoyenye ushindani mkubwa.

"Narudi nyumbani ndani ya wiki hizi, mama yangu anaumwa, lakini msimu huu umekuwa bora sana kwangu, nimepata nafasi ya kucheza nikiwa kwenye ligi ngumu," amesema Zizou na kuongeza;

"Tamanio langu ilikuwa kucheza ligi ya mabingwa Afrika na nashukuru tumefanikiwa, ingawa inaweza kuwa ngumu kwangu kucheza kwa sababu narudi nyumbani kumuuguza mama."

Mogbwemo Queens ilibeba taji hilo mapema baada ya Ram Kamara inayoshika nafasi ya pili kukatwa pointi tano kwa kosa la kuchezesha wachezaji watano wa kigeni kinyume na kanuni za ligi hiyo.

Kupunguzwa kwa pointi hizo kuliwapa nafasi Mogbwemo Queens kujihakikishia ubingwa bila kusubiri matokeo ya mechi zilizobaki.