Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yampiga mtu 9 huko Avic, Mayele atetema tena

YANGA imecheza mchezo wa pili wa kujipima nguvu wakishusha kipigo kizito kwa Friends Ranger wakishinda kwa mabao 9-0.

Mchezo huo ambao umepigwa leo asubuhi mshambuliaji Fiston  Mayele ameendelea kutetema akipiga bao moja katika mchezo huo huku Lazarous Kambole naye akifungua akauti ya mabao.

Mabao mengine yamefungwa na kiungo Khalid Aucho na mshambuliaji kinda kutoka timu B Clement Francis wote wakifunga mara mbili kila mmoja.

Wengine waliocheka na nyavu katika ushindi huo ni pamoja na winga Denis Nkane, Jesus Moloko na Yacouba Sogne kila mmoja akifunga bao moja katika mchezo huo ambao Yanga walionekana kutawala.

Huo unakuwa ni ushindi wa pili wa Yanga ndani ya wiki moja tangu waanze kambi yao ya maandalizi ya msimu ambapo Julai 29 walicheza dhidi ya Transit Camp ambapo mabingwa wao walishinda kwa mabao 5-1.