Yanga yambeba Mudathir, yaipiga bao Simba
Yanga imeanza usajili wa dirisha dogo kibabe baada ya kumtangaza kiungo mkabaji Mudathir Yahaya.
Mudathir ambaye ni kiungo wa zamani wa Azam amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga ambayo ni mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi.
Mudathir anaungana na mastaa wenzake wa Azam winga Farid Mussa na kiungo Salum Aboubakar 'Sure boy.
Usajili huo unaifanya Yanga Sasa kuwa na viungo wanne wa ukabaji wakiwemo Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Gael Bigirimana na kiraka Yannick Bangala.
Yanga imeipiga bao Simba katika usajili huo ambao nao waliwahi kutamani huduma ya kiungo huyo Mzanzibar, ambaye hakucheza miezi sita Ligi Kuu Bara baada ya kuachana na Azam.
Huyo anakuwa mchezaji wa kwanza mpya kwa Yanga kumsajili katika dirisha dogo huku wengine wawili watatu wakifuatia ingawa uongozi wa klabu hiyo unafanya siri.