Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yacheza dakika 120, ikimpiga mtu 2-1

Muktasari:

  • Katika kupima pumzi ya wachezaji wake, kocha wa Yanga, Romain Folz akawataka Fountain Gate kucheza nao kwa dakika 120.

YANGA imecheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Fountain Gate ikishinda kwa mabao 2-1, leo Agosti 23, 2025 kwenye Uwanja wa KMC Complex jijini Dar.

Katika kupima pumzi ya wachezaji wake, kocha wa Yanga, Romain Folz akawataka Fountain Gate kucheza nao kwa dakika 120.

Akili ya Folz ni kutaka kupima vifua vya wachezaji wake kuhimili dakika zaid ya 90 baada ya mazoezi yao ya pumzi na stamina.

Mchezo huo ulikuwa na vipindi vitatu tofauti, vilivyogawanywa kwa dakika 40 kila kimoja.

Yanga imekuwa kwenye mazoezi hayo magumu kwa wiki nzima ikianzia ufukweni na kisha kukimbia uwanjani kule kambini kwao Avic Town, Kigamboni.

Kwenye mchezo huo kocha wa Yanga amekuwa akiwapa nafasi wachezaji wake tofauti akiwapima kila kitu ambacho wasaidizi wake, walikuwa wakirekodi mambo tofauti.

Kwenye mchezo huo mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo Aziz Andambwile na mshambuliaji Prince Dube huku lile la Fountain likifungwa na Camara ambaye anafanya majaribio na timu hiyo.