Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga waendeleza ubabe kwa maafande JKT

Muktasari:

Ushindi wa mabao 2-0 walioupata Yanga mbele ya maafande wa JKT Tanzania, umeendeleza rekodi nzuri ya Yanga kila wakikutana na JKT.

Dodoma. Ushindi wa mabao 2-0 walioupata Yanga mbele ya maafande wa JKT Tanzania, umeendeleza rekodi nzuri ya Yanga kila wakikutana na JKT.

Ushindi huo uliopatikana kupitia mabao ya Yacouba Songne na Tuisila Kisinda, kwenye Kipindi cha kwanza, umewafanya Yanga waimarishe rekodi hiyo nzuri mbele ya maafande hao.

Huu ulikuwa ni mchezo wa 15 tangu mwaka 2013, Yanga ikifanikiwa kuandikisha rekodi ya kushinda mchezo wa 14 na sare moja pekee.

Sare ya mwisho kwa timu hizo ni wa mchezo wa msimu uliopita, uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini hapa, ambapo walitoshana sare ya bao 1-1.

Ubora wa Yanga kwenye eneo la kiungo ndilo lililoipa ushindi huo muhimu kwa Yanga, katika harakati zao za kusaka ubingwa dhidi ya Simba wanaoongoza.

Kiungo cha Yanga kilichoongozwa na Mukoko Tonombe na Feisal Salum wakisaidiwa vema na wale wa pembeni, Tuisila Kisinda na Ditram Nchimbi, uliwapoteza kabisa maafande wa JKT Tanzania.

Hata wakati wakiongoza kwa mabao mawili, Kocha Nasreddine El Nabi, aliwaingiza viungo Deus Kaseke, Zawadi Mauya ambao waliongeza ufanisi wa eneo hilo.

Ushindi huo kwa Yanga umewafanya wafikishe alama 61, sawa na walizonazo Simba, wakipishana idadi ya mechi za kucheza.

Kocha wa JKT Tanzania, Abdallah Mohamed 'Bares' alisema kuwa vijana wake walishindwa kuhimili kasi ya Yanga iliyopelekea kupoteza mchezo huo, huku akiwapongeza kwa kubadilika kipindi cha pili.

"Tumepoteza mchezo, tulishinda kucheza vema kipindi cha kwanza na Yanga wakatufunga, kipindi cha pili walicheza vema" alisema Bares.

Razack Siwa, Kocha wa makipa wa Yanga alisema ushindi huo umeongeza imani yao ya kubeba ubingwa wa ligi kuu.

"Ushindi huu tuliupangilia vema na ilikuwa na lengo la kushinda na tumefanikiwa, bado tunaamini tunaweza kubeba ubingwa" alisema Siwa.

Imeandikwa Matereka Jalilu