Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga Tandale wadai Tumewanyoosha TFF

Muktasari:

BAADA ya Yanga kuamua kutimka na kususa mechi dhidi ya watani wao wa jadi Simba, wanachama wa klabu hiyo wamesema hilo ni onyo kwa TFF ambayo imekuwa ikifanya mambo kiholela bila kufuata kanuni.

BAADA ya Yanga kuamua kutimka na kususa mechi dhidi ya watani wao wa jadi Simba, wanachama wa klabu hiyo wamesema hilo ni onyo kwa TFF ambayo imekuwa ikifanya mambo kiholela bila kufuata kanuni.

Jumamosi iliyopita Yanga iligomea kucheza na Simba saa 1:00 usiku baada ya muda wa awali wa saa 11:00 kubadilishwa huku sababu zikishindwa kuwekwa wazi.

Katibu wa tawi la Yanga Mwamko Tandale sokoni, Said Mwalutambi alisema Yanga wala hawakuogopa mechi hiyo lakini walifuata sheria ili kuwakomesha TFF.

“TFF walipotoa taarifa ya kusogezwa muda wa mechi hawakusema sababu hilo ndilo walilokosea, hawawezi kubadilisha muda wa mechi kienyeji.

“Yanga hatukuogopa mechi ila tulifanya vile ili kuwakomesha TFF kuwa wanatakiwa kufuata sheria na kanuni za mchezo kwani mara kwa mara wamekuwa wanabadilisha ovyo ratiba za mechi,” alisema Mwalutambi.

Mwalutambi alisema kutokana na kosa hilo viongozi wa TFF na hata wizara ya michezo wanatakiwa kuwajibika kwani wamesababisha taharuki kwa mashabiki ambao walilipa viingilio vyao ili kuona mchezo.

Katibu huyo alisema wako tayari kucheza mechi nyingine kwa tarehe itakayopangwa kwani wanaamini wana kikosi bora kitakachoweza kuibuka na ushindi siku hiyo.

Tawi hilo la Mwamko lilianzishwa Novemba mwaka jana na lina wanachama 120 huku likiongozwa na Mwenyekiti, Majid Kingilingili, makamu ni Osward Miti, Katibu ni Mwalumbati wakati mtunza hazina ni Omari Sharifu.