Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Simba zafuzu Ligi ya Mabingwa

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na pointi 69 huku Simba ikifuata na pointi zake 67.

Yanga na Simba zimekata rasmi tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao baada ya kila moja kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi zilizocheza dhidi ya timu za Azam na Mtibwa Sugar kwenye viwanja tofauti leo.

Yanga ambayo imeibuka na ushindi dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, imefikisha pointi 69 na Simba ambayo imeichapa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro, imefikisha pointi 67, pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 16 kwenye Ligi msimu huu.

Hata hivyo, Azam na Singida Black Stars nazo zimejihakikishia kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Ibrahim Abdullah ‘Bacca’, Pacome Zouzoua na Laurindo Dilson ‘Depu’.

Simba kwa upande wake imepata mabao yake kupitia kwa Rushine De Reuck, Selemani Mwalimu na Anicet Oura.

Katika Uwanja wa Airtel Singida, wenyeji Singida Black Stars wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Pamba Jiji FC imesulubiwa na Mbeya City nyumbani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ikichapwa mabao 2-0.

Matokeo hayo yameifanya Tanzania Prisons ishuke hadi nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi huku Mbeya City ikipanda hadi nafasi ya 13.

Mtibwa Sugar imeshuka kwa nafasi moja hadi nafasi ya 14.


Matokeo ya mechi za leo

Yanga 3-0 Azam

Mtibwa 0-3 Simba

Singida BS 3-1 Tanzania Prisons

Pamba Jiji 0-2 Mbeya City

TRA United 1-1 Coastal

Dodoma Jiji 0-0 JKT Tanzania

Fountain Gate 0-1 Mashujaa

KMC 2-3 Namungo