Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga ruksa kusajili

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeiondolea klabu ya Yanga adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kumlipa mchezaji Gael Bigirimana.

Bigiramana alikuwa mchezaji wa Yanga, alifungua kesi FIFA baada ya timu hiyo kushindwa kumlipa baada ya kumvunjia mkataba.

"Bigirimana alishinda kesi hiyo, na Yanga ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa, lakini haikutekeleza na kusababisha ifungiwe kusajili," imeeleza taaifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

TFF pia imeeleza kuwa imefungulia Yanga kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Desemba 16 na kufungwa Januari 15.