Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga pesa yenu tu kwa Luhende

Muktasari:

Luhende aliyebakiza miezi michache kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na Mtibwa, amesema wala hana tatizo na Yanga, pesa yao tu.

YANGA ipo katika mkakati wa kuhakikisha inamrudisha kundini beki wa kushoto, David Luhende, kutoka Mtibwa Sugar.

 Luhende aliyebakiza miezi michache kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na Mtibwa, amesema wala hana tatizo na Yanga, pesa yao tu.

Luhende aliondoka Yanga kabla ya kuanza kwa msimu huu baada ya uongozi kushindwa kumpa mkataba mpya, kikosini Mtibwa amekuwa akifanya vizuri na kupitia mmoja wa viongozi wake, Yanga imeanza mipango ya chinichini kuhakikisha Luhende anarudishwa kikosini ili kusaidiana na Oscar Joshua.

Juu ya hilo, Luhende amesema: “Naelekea kumaliza mkataba wangu Mtibwa, si Yanga tu, timu yoyote ije tuzungumze cha kufanya, mpira ndio kazi yangu.”