Yanga mpya bila Mwenyekiti wala Makamu, TFF yatoa miezi sita

Yanga yaipongeza Simba, yatamba kunyakua yaliyobaki

MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema mchakato wa kuingia kwenye mabadiliko kwa klabu yao haukuwa rahisi kwa walipofikia kilichobaki ni utekelezaji.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mbatha alisema tayari Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limeshapotisha katiba yao ambayo itaifanya timu yao iendeshwe kisasa huku akitasha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwapa miezi sita ili waweze kufanyia kazi kile walichokiandaa kwenye katiba yao mpya.

Alisema mchakato wao wa mabadiliko hautokuwa na nafasi ya Makamu wala Mwenyekiti wa klabu wanaiendesha klabu kisasa kwa kuwa na Rais.

“Hatutokuwa na Mwenyekiti wala Makamu Mwenyekiti kwenye muundo mpya wa klabu ya Yanga,” Senzo

“TFF wametupa miezi sita kufanya kile ambacho kipo kwenye katiba yetu mpya”, Senzo

“Kila Mwanachama wa Yanga anatakiwa awe na tawi lake, huwezi kuwa mwanachama kama hauna tawi na ndio maana unatakiwa ujisajili kwenye tawi,” Senzo

“Tunaleta kampuni maalum yenye weledi itakayokuja kutupa thamani halisi ya klabu na sio ile ya uongo ili kuleta picha halisi ya mabadiliko tunayokwenda kuyafanya”, Senzo