Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga kuvuta winga Bamako

Muktasari:

  • Yanga itakuwe wenyeji wa Bamako katika mechi ya Kundi D ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayopigwa Jumatano ijayo jijini Dar es Salaam baada ya wikiendi iliyopita kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Machi 26, jijini Bamako Mali.

KIKOSI cha Yanga usiku wa juzi kilikuwa uwanjani kumalizana na Tanzania Prisons katika mechi ya Kombe la Shirikisho (ASFC) hatua ya 16 Bora, huku mabosi wao wakikuna kichwa kwa ajili ya kuibomoa Real Bamako ya Mali wanaotarajiwa kuwa wageni wao kwa mechi za CAF.

Yanga itakuwe wenyeji wa Bamako katika mechi ya Kundi D ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayopigwa Jumatano ijayo jijini Dar es Salaam baada ya wikiendi iliyopita kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Machi 26, jijini Bamako Mali.

Sasa unaambiwa, dakika 52 alizocheza winga wa Bamako, Cheickna Diakité mwenye umri wa miaka 18 dhidi ya Yanga imemfanya wakati wowote anaweza kuwa staa mpya wa Jangwani kwani kwa sasa amebakiza hatua moja tu kuingia kwenye mikono ya klabu hiyo baada ya Kocha Nasreddine Nabi kubeba faili lake.

Yanga ikiwa ugenini dhidi ya Real Bamako mabosi wake walivutiwa na kazi ya Diakite aliyewasumbua mabeki wa Yanga katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1 wenyeji wakichomoa bao dakika la salama baada ya awali Fiston Mayele kuwatanguliza wawakilishi wa Tanzania.

Baada ya mchezo huo Mwanaspoti linafahamu kuwa bosi mmoja wa juu wa Yanga aliteta na staa huyo kisha kuchukua taarifa zake juu ya mkataba wake na Bamako kabla ya kufanya maamuzi.

Winga huyo ndani ya dakika 52 alizokuwa uwanjani alionekana kumpa wakati mgumu beki Djuma Shaban kutokana na kasi yake na ufundi wake kabla ya kutolewa kipindi cha pili akiingia Chaka Sidibe, aliyepiga kona iliyozaa bao la kusawazisha la wenyeji lililofungwa kwa kicha na Emile Kone.

Hata hivyo, mabosi wa Yanga wanataka kujipa muda zaidi na kumpa pia nafasi kocha Nabi na jopo lake kumsoma zaidi Diakite katika dakika 90 za mechi ya marudiano Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya kufanya maamuzi yatakayozidi kuijenga timu hiyo.

"Alicheza vizuri ule mchezo wa kwao tumeongea naye vizuri lakini ngoja waje hapa kuna vitu ambavyo tunataka kujiridhisha zaidi kabla ya kufanya maamuzi," alisema bosi huyo (jina tunalo) na kuongeza;.

"Hatutaki kufanya maamuzi ya haraka, lengo letu tupate watu muafaka zaidi wa eneo hilo, unajua eneo hili la mawinga nalo limetuangusha sana tuliwarudisha Morrison (Bernard) na Kisinda (Twisila) lakini bado hawajatupa kile ambacho tulikilenga.

"Tunataka kuanza mapema hesabu hizi ili tufanye maamuzi yenye afya kwa timu yetu kwa msimu ujao na tunataka kutumia mechi kama hizi za Kimataifa kuchagua watu bora ambao watakuja kutongezea thamani ya kikosi chetu."

Mapema Mwanaspoti linafahamu kuwa katika dirisha kubwa la usajili kuna uwezekano mkubwa wakafumua idara yao ya mawinga wa pembeni kwa kuleta watu wa maana baada ya waliopo sasa kuonyesha kiwango ambacho benchi lao la ufundi halijakubaliana na viwango vyao.

Kwa sasa Yanga inayoongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 62 baada ya mechi 23 na kushika nafasi ya pili ya Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika ina mawinga wasiopungua sita akiwamo Tuisila, Farid Mussa, Jesus Moloko, Dickson Ambundo, Denis Nkane na Morrison ambaye kwa muda mrefu haonekani uwanjani.