Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wolper, Hamornize watibuana Instagram

Muktasari:

  • Wawili hao waliowahi kuwa wapenzi, Wolper na Hamornize wametupiana maneno makali ya vijembe katika kurasa zao za Instagram, baada ya habari kuvuja kwenye mitandano ya kijamii zikidai yule demu Mzungu wa Harmonize anayeitwa Sarah, amemtosa Harmonize na kumchukua Bodyguard wa Diamond Platinumz, anayejulikana kwa jina la Mwarabu Fighter.

Siku mbili zilizopita, kumeibuka na mtafaruku baina ya Jacqueline Wolper na mwanamuziki Hamornize baada ya kurushiana vijembe mtandaoni.

 

Wawili hao waliowahi kuwa wapenzi, Wolper na Hamornize wametupiana maneno makali ya vijembe katika kurasa zao za Instagram, baada ya habari kuvuja kwenye mitandano ya kijamii zikidai yule demu Mzungu wa Harmonize anayeitwa Sarah, amemtosa Harmonize na kumchukua Bodyguard wa Diamond Platinumz, anayejulikana kwa jina la Mwarabu Fighter.

 

Habari zinadai kuwa Sarah amezimika kwa Mwarabu Fighter hadi kufikia hatua ya kumpangishia nyumba na huduma zozote alizokuwa anapata Harmonize amezihamishia kwa mlinzi huyo wa Diamond.

Sarah na Wolper wamekuwa kwenye vita ya mapenzi huku ikidaiwa chanzo ni penzi la Harmonize, lakini baada ya tetesi hizo za usaliti kusambaa mitandaoni. 

 

Baada ya kipande cha video ya mahojiano ya Wolper kusambaa katika mitandao ya kijamii, Hamornize alimtetea Mzungu wake kwa kumjibu Wolper kupitia akaunti yake ya Instagram, huku akiorodhesha wanaume aliowahi kutoka nao kimapenzi.

 

 

Soma gazeti la Mwanaspoti kesho kupata habari hii kwa kina jinsi ambavyo Wolper amefunguka baada ya mahojiano na mwandishi.