Wawekezaji wanne kugawana hisa asilimia 49 Yanga

Wawekezaji wanne kugawana hisa asilimia 49 Yanga

Arafat Haji anayegombea nafasi ya makamu wa rais kwenye uchaguzi mkuu wa Yanga amesisitiza kwamba wawekezaji wanne watagawana asilimia 49 za hisa kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

Amesema kila mwekezaji atapewa asilimia 12.25 katika asilimia 49 za hisa kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa kampuni.

Arafat ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa klabu hiyo inayowaniwa na Injinia Hersi Said leo Julai 5, kwenye hoteli ya Serena Dar es Salaam.

"Klabu imeweka utaratibu mzuri kwenye mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji, tutakuwa na wawekezaji wanne ambao watagawana asilimia 49 ya hisa," amesema Arafat ambaye sasa ni mwenyekiti wa kamati ya fedha ya klabu hiyo.