Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji wapya watua Simba, wawili kukatwa

Muktasari:

Usajili wa wachezaji hao ndani ya kikosi cha Simba, lazima klabu hiyo ifanye maamuzi magumu ya kupunguza sehemu ya wachezaji 10, wa kigeni walionao sasa hivi.

Dar es Salaam. Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi Klabu ya Simba, imeshusha majembe mawili ya maana huku lingine likitarajiwa kuingia muda wowote kuanzia sasa.
Majembe hayo si ya kulimia bali ni wachezaji ambao wamekuja kufanya majaribio ili waweze kuichezea timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni beki wa kati, Mghana Moro Lamine na straika Mtogo Hunlede Kissimbo Ayi walianza kufanya mazoezi na Simba leo Jumatatu jioni katika Uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es Salaam chini ya uangalizi wa Kocha Patrick Aussems ambaye ndiye atakayetoa kauli ya mwisho juu ya usajili wao wapewe mikataba au wafyekelewe mbali.
Si hao tu, mabosi wa Simba katika kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao zaidi, straika mwingine kutoka nchini Namibia anatarajiwa kuingia muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya majaribio kama hayo.
"Hawa wachezaji tumewaleta kwa ajili ya majaribio na si hawa wawili tu bali watakuwa watatu na mwingine straika kutoka Namibia mtamuona siku si nyingi atawasili nchini," alisema mmoja wa kigogo wa Simba ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.
"Tutawatumia wachezaji hawa katika mashindano ya SportPesa na itakuwa kama sehemu yao ya majaribio ili kuona kama wanauwezo wa kuisaidia Simba ili tuwasajili na kama watakuwa hawana uwezo kwa mujibu wa kocha wetu tutaachana nao," alisema.