Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Yanga yasajili 32, viungo 12, washambuliaji 9

Muktasari:

  • Yanga imetangaza orodha ya wachezaji wake iliyowasajili wakiwa 32, hiyo ni baada ya kushindwa kuwatoa kwa mkopo kipa wake Youthe Rostand na kiungo Pato Ngonyani kwa African Lyon katika dakika za mwisho.

Dar es Salaam. Presha na usajili wa lala salama umeifanya Yanga kusajili wachezaji 32 badala ya 30, huku wakiweka rekodi ya kusajili viungo 12 na washambuliaji tisa na mabeki saba.

Yanga imetangaza orodha ya wachezaji wake iliyowasajili wakiwa 32, hiyo ni baada ya kushindwa kuwatoa kwa mkopo kipa wake Youthe Rostand na kiungo Pato Ngonyani kwa African Lyon katika dakika za mwisho.

Kanuni za usajili zinataka kila timu hadi jana saa 6 usiku iwe na wachezaji 30 au chini ya hapo ikiwa ni pamoja na wale wa mkopo.

Mbali ya kasoro hiyo Yanga imejiweka katika wakati mgumu zaidi msimu huu hasa katika safu yake ya ulinzi baada ya kusajili wachezaji saba tu.

Mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Bara wamesajili viungo 12, msimu huu na washambuliaji tisa katika kuhakikisha inatatua tatizo la ukama wa mabao.

Kikosi cha Yanga

Makipa: Youthe Rostand, Ramadhan Kabwili, Beno Kakolanya, Klaus Kindoki

Mabeki: Juma Abdul, Mwinyi Haji, Gadiel Michael, Kelvin Yondan, Andrew Vincent, Abdallah Shaibu, Cleofas Sospeter

Viungo: Papy Kabamba, Kamusoko Thaban, Raphael Daud, Maka Edward, Said Makapu, Feisal Salum, Deus Kaseke, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, Pato Ngonyani, Paulo Godfrey.

Washabuliaji: Matheo Anthony, Mrisho Ngassa, Amis Tambwe, Ibrahim Ajib, Heritier Makambo,Yusuph Mhilu, Baruan Akilimali, Said Mussa, Yohanna Mkomola.