Ushuhuda wangu kwa Mbwana Samatta 4- Udereva ulimpa wakati mgumu Ubelgiji

Muktasari:
Maswali yale niliyokuwa na waandishi mbalimbali kule Genk miaka minne iliyopita nadhani ni leo anaweza kuulizwa mwandishi yeyote wa kwanza wa Tanzania atakayefika kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa waandishi wa habari wa uwanja wa Villa Park pale Birmingham.
Jaribu kufikiria pia, kesho yake Samatta alifuatwa nyumbani na gari la klabu, aina ya Marcedes Benz saa tisa alasiri. Mechi ilikuwa inaanza saa 12. Hapa ndio utajua namna ambavyo wenzetu wanaishi kama wanasoka wa kulipwa hasa.
Nilikwenda uwanjani kama mwandishi wa habari. Huduma za waandishi wa habari Ulaya ni za hali ya juu. Katika ukumbi wa waandishi wa habari waliokuwa wanaripoti mechi hiyo wengi walikuwa wananiulizia kuhusu Samatta na Tanzania yake.
Hadi kufikia mechi hiyo Samatta alikuwa ameshaonyesha makali yake na waandishi walionekana kutaka kujua maisha ya Samatta kabla ya kufika Genk, walitaka kujua kama Tanzania ni nchi ya soka, walitaka kujua kama kuna vipaji, walitaka kujua mengi.
Maswali yale niliyokuwa na waandishi mbalimbali kule Genk miaka minne iliyopita nadhani ni leo anaweza kuulizwa mwandishi yeyote wa kwanza wa Tanzania atakayefika kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa waandishi wa habari wa uwanja wa Villa Park pale Birmingham.
Katika pambano hilo dhidi ya Oostende Samatta alitupia bao moja la kichwa. Genk walishinda 4-1. Hata hivyo kuna kitu kimoja kiliniumiza kichwa. Lakini pia kumbe ni kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza kichwa Samatta pia.
Baada ya pambano kumalizika nilipata nafasi ya kuwa karibu na wachezaji wa Genk wa wakati huo. Niliongea kidogo na Leon Bailey, winga wa kimataifa wa Jamaica ambaye wakati huo alikuwa na miaka 18 tu.
Niliongea pia na Wilfried Ndidi, kiungo wa kimataifa Nigeria ambaye wakati huo alikuwa na miaka 20. Hawa walionekana kuwa watu wa karibu wa Samatta katika kikosi kile cha Genk ambacho kwa sasa wote wamesambaratika.
Kwa sasa Bailey yupo Bayer Leverkusen baada ya kutakiwa na klabu mbalimbali kubwa Ulaya. Ndidi kama tunavyomuona yupo na Leicester City. Kilichokuwa kinamuumiza Samatta ni namna ambavyo alipoteza muda mwingi pale Congo. Aliingia Genk akiwa na umri wa miaka 23 wakati wenzake wengi walikuwa chini ya umri wa miaka 20.
Alikuwepo pia Christian Kabaselle ambaye kwa sasa anatamba na Watford na ameanza kusakwa na klabu mbalimbali kubwa za barani Ulaya.
“Brother yaani natamani ningekuwa na miaka kama 18 hivi aisee. Nimepoteza sana muda mpira wa Afrika,” aliniambia Samatta nyakati hizo.
Wakati huo Samatta hakuwa Samatta huyu wa juzi. Wakati huo wimbo wa Samagoal haukuwepo. Alikuwa kijana wa Kiafrika aliyeanza kutengeneza himaya yake Genk. Sawa alikuwa anafunga mara kwa mara lakini hakuwa kama huyu hapa ambaye ameuzwa kwenda Aston Villa.
Wakati huo Samatta alikuwa na nafasi nzuri ya kuanza mechi lakini hakuwa panga pangua kikosini. Genk pia walikuwa wamemnasa mshambuliaji mahiri wa Kigiriki, Nikos Karelis ambaye naye alikuwa na sifa ya kuziona nyavu.
Nilipoenda katika duka la klabu hiyo kwa mara ya kwanza jezi yake namba 77 ya wakati huo ilikuwa inauzika kama zilivyo jezi za mastaa wengine klabuni hapo. hakuwa mtu maalumu kama niliyemkuta wakati nilipokwenda klabuni hapo kwa mara ya pili.
Nje ya uwanja, Samatta niliyemkuta katika safari yangu ya kwanza alikuwa na changamoto nyingine mbalimbali. Kwa mfano, hakuruhusiwa kuendesha gari na alilazimika kupelekwa kufanya mitihani mbalimbali ya namna ya kuendesha na kuzingatia sheria za uendeshaji za