Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UKISIKIA PAA!

Muktasari:

Kutokana na kiwango kilichoonekana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, benchi la ufundi la Simba huenda likafanya mabadiliko makubwa ili kuanza michuano hiyo na mguu mzuri kwani Yanga ambao kesho watacheza na Lipuli watakuwa jukwaani wakiwachabo tu.

UKISIKIA PAA! Ujue shoo imeanza na muda wa kutesti mitambo na kufanya mbwembwe umekwisha. Sasa ni kazi tu Simba itaanzia msimu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo Jumamosi ikitumia kikosi chake cha Sh 1.3 bilioni kuikabili Ruvu Shooting ya Pwani ambayo gharama za usajili wake wote hazitoshi kumnunua Haruna Niyonzima.

Kutokana na kiwango kilichoonekana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, benchi la ufundi la Simba huenda likafanya mabadiliko makubwa ili kuanza michuano hiyo na mguu mzuri kwani Yanga ambao kesho watacheza na Lipuli watakuwa jukwaani wakiwachabo tu.

Rekodi zinaonyesha Ruvu haijapata ushindi wowote dhidi ya Simba katika mechi nane zilizopita, ambapo matokeo yao mazuri zaidi kwao ni sare ya bao 1-1 iliyopata Oktoba 5, 2013 lakini imefungwa katika mechi saba.

“Naweza kufanya mabadiliko machache kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Yanga,” alisema kocha wa Simba, Joseph Omog. Kocha wa zamani wa makipa wa Simba, Iddi Pazi amemshauri Omog kuwa makini na wachezaji maarufu wasiofanya vizuri.

“Kuna wachezaji wakubwa ambao hawapendi kukaa benchi, lakini kama hawatoi matokeo unafanyeje?” Alisema.

Ruvu imepata pigo kwa kuwakosa mastraika wake tegemeo, Fully Maganga aliye majeruhi na Abdulrahman Mussa aliyeenda Burundi kwenye mashindano ya Majeshi kwa Afrika Mashariki.

YANGA HAIJAPOTEZA

Kabamba Tshishimbi atakuwa jukwaani leo akiicheki Simba freshi. Wao mechi yao wanaanza kesho Jumapili na timu ngeni ya kutoka Iringa, Lipuli FC iliyopo chini ya nyota wa zamani wa Simba, Selemani Matola.

Rekodi zinaonyesha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Yanga haijawahi kupoteza mchezo wowote nyumbani kwa timu kutoka nje ya Dar es Salaam. Timu ya nje ya Dar iliyopata matokeo mazuri dhidi ya Yanga ni Ndanda ya Mtwara ambayo iliambulia suluhu Januari 31, 2015.

“Tunawaheshimu Yanga kama watetezi, ni changamoto kubwa kwetu kuanza ligi dhidi yao. Tutacheza kwa nidhamu kubwa kuona tunachoweza kupata,” alisema kocha Matola ambaye Simba wanamuita Kapteni.

SINGIDA HAWA

Kocha fundi anayeaminika zaidi katika kuusoma mchezo, Hans Pluijm akiwa na kikosi chake cha gharama kubwa ataivaa Mwadui FC mjini Shinyanga.

Singida imesajili wachezaji 16 wapya ikiwemo saba wa kigeni na kocha Pluijm aliyewahi kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga, amepania mno.

Hata hivyo Mwadui wameweka ngumu na kudai kwamba hawatakubali kuwa sehemu ya uchochoro wa timu hiyo inayotembelea basi la Sh350 milioni.

“Tunafahamu Singida inacheza soka la kushambulia sana, kwetu hilo siyo tatizo kubwa, nasi tutawashambulia.

Tutacheza kwa kusimamia misingi yetu na kubadilika kulingana na mechi,” alisema Kaimu Kocha wa Mwadui, Khaleed Adams, ingawa Pluijm amesisitiza kwamba yeye ataonyesha kazi yake uwanjani na hana wasiwasi wote.