Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukipona kwa BBS ya Yanga katambike

Muktasari:

BBS ilionyesha ubora wa hali ya juu huku wakichezea mipira na kupigiana pasi za mwisho kwa ufundi na kufika kwenye lango la adui wakifanya mashambulizi ya hatari.

Morogoro. Simba wanaendelea kujipanga kule Bondeni, lakini Yanga wenyewe wamejichimbia pale Mji kasoro bahari, Morogoro. Ndani ya siku kadhaa walizojificha kwenye kambi yao iliyopo Bigwa, ulinzi ulikuwa wa kufa mtu ambapo hata baadhi ya vigogo walizuiwa kutazama mazoezi na kuzungumza na wachezaji.
Lakini, imebainika kuwa kuna mambo mazito yalikuwa yakipikwa na sasa Mwanaspoti linakumegea kwamba, ile fomesheni iliyokuwa ikitafutwa ndio imepatikana. Achana na ile ya MSN ya Barcelona (Messi, Suarez na Neymar) ama BBC ya Real Madrid (Bale, Benzema na Ronaldo) ambazo zote zimesambaratika huku Yanga kuna BBS.
Kombinesheni hiyo inahusisha washambuliaji hatari ambao wote wapya walionaswa msimu huu, Juma Balinya (JB), Issa Bigirimana na Patrick Sibomana ambayo imepewa jina la BBS.
Tayari ndani ya kikosi cha Yanga kuna ari kubwa kwa wachezaji wake huku kazi ya kuendelea kusuka kombinesheni zingine ikiendelea kwa kasi chini ya benchi la ufundi kwa maelekezo ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.
Juzi Yanga ilicheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Moro Kids iliyochanganyika na vijana wa Mtibwa Sugar waliochukua ubingwa wa vijana hivi karibuni na matokeo yalikuwa ni ushindi wa mabao 2-0. Shukrani kwa Balinya na beki wa kulia, Paul Godfrey. Katika mchezo huo kocha Noel Mwandila alianza na washambuliaji Juma Balinya kati, akisaidiana na Bigirimana wakati winga ya kulia akiwa mkongwe Mrisho Ngassa na kushoto akachukua Sibomana.
Ndani ya dakika 45 tu kombinesheni ya BBS ikajipambanua mbele ya benchi la ufundi na mashabiki waliohudhuria mchezo huo.
Pale kati Mwandila akampa nafasi Feisal Salum ‘Fei Toto’ akisaidiana kazi na Mohamed Issa ‘Banka’ beki ya kulia akachukua Boxer na kushoto akapewa Muharami Issa ‘Marcelo’.
Beki ya kati ilikuwa chini ya kinda Cleophas Sospeter akisaidiana na Mustapha Seleman huku langoni akasimama Metacha Mnata. BBS ilionyesha ubora wa hali ya juu huku wakichezea mipira na kupigiana pasi za mwisho kwa ufundi na kufika kwenye lango la adui wakifanya mashambulizi ya hatari.

Balinya si mtu mzuri
Balinya katika mchezo huo alipiga mashuti matano huku matatu yakilenga lango akipachika bao moja la penalti dakika ya 45 kufuatia Sibomana kuangushwa eneo la hatari.
Kabla ya kuangushwa kwa Sibomana alikuwa mwiba mkali akishirikiana vyema na Balinya na Bigirimana huku Ngassa na Fei Toto wakiongeza nguvu kwa nyuma. Ilikuwa kama wanapishana ambapo wakati Sibomabana akitulia, Bigirimana naye alikuwa akiibuka na kufanya mashambulizi huku kitu hatari zaidi ni kubadilishana kwao nafasi kila baada ya dakika 10 na kuwachanganya mabeki wa Moro Kids. Kitu hatari zaidi kwa Balinya ni kuwa na nguvu na kasi, lakini kubwa ni uwezo wake wa kufunga.
Baadaye Mwandila aliamua kuipumzisha BBS na kuwaingiza Deus Kaseke, Raphael Daud na Yanga haikufanikiwa kupata bao na mchezo kumalizika kwa matokeo hayo. Endapo Bigirimana, Balinya na Sibomana (BBS) wakiendelea kucheza pamoja, basi kama wapinzani wao watatoka salama uwanjani wakatambike kutokana na kasi na ujanja wa kupenyeza mipira langoni mwa adui.

Msola aisoma timu
Pale nje Yanga ikitoa dozi hiyo, Mwenyekiti wao Mshindo Msolla alikuwa amekaa benchi akiusoma mchezo kwa dakika zote kisha kutoa neno.
“Nimeona timu kuna kitu kizuri kinakuja,” alisema Msola.