Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukata waizuia Majimaji kwenda Kigoma

BAADA ya kushindwa kusafiri kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa play off dhidi ya Kasulu United, uongozi wa muda wa Majimaji FC umesema unasubiri maamuzi yoyote kutoka mamlaka za soka nchini.
Majimaji ilipaswa kusafiri mkoani Kigoma kukamilisha ratiba ya mchezo wa mchujo hatua ya pili ‘play off’ dhidi ya wapinzani hao, lakini licha ya kupangiwa tarehe mara kwa mara hali imeendelea kuwa ngumu.
Katika mchezo wa awali, ‘Wanalizombe’ hao wakiwa nyumbani walishinda bao 1-0 na walipaswa kurudiana na wapinzani Aprili 18, lakini hawakusafiri kisha kuomba isogezwe hadi 21, baadaye 27 lakini hawakutokea.
Katibu mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Songea (Sodfa), God Mvula ambao ndio wameishikilia kwa sasa baada ya waliokuwa viongozi wake kuikacha timu, alisema baada ya kushindwa kusafiri wanasubiri maamuzi yatakayotolewa.
Alisema changamoto bado ni ile ile ya ukata ambao imewafanya kutoweza kufika mkoani Kigoma kukamilisha ratiba na kwamba wanasubiri aidha kucheza dhidi ya timu za ligi ya mabingwa wa Mikoa (RCL) au kushushwa daraja.
“Hali bado haijatulia licha ya kufanikiwa kuikarabati gari la timu ila gharama za safari hazijapatikana, tunasubiri lolote litakalotokea ikiwa ni kushushwa au kucheza play off na timu ya RCL sawa,”
“Changamoto ya wadau mkoani hapa wanapenda mpira ila hawako tayari kuchangia, unakuta watu wanalalamikia matokeo na mwenendo wa Majimaji, lakini hawana sapoti yoyote,” alisema Mvula.
Mdau wa soka mkoani humo, Raphael Njunwa alisema timu hiyo ilianza kupoteana kuanzia kwenye uongozi ambao ulishindwa kuweka mipango kama ilivyokuwa awali.
“Zamani Majimaji ilikuwa na wadau wake maalumu wa kusapoti lakini uongozi wa sasa unafanya mambo yao kivyao hakuna ushirikiano hivyo inakuwa ngumu kuichangia,” alisema Njunwa.