Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA United v Simba waahirishwa, kupangwa siku nyingine

Muktasari:

  • Akizungumza na Azam TV, Kamishna wa mchezo huo Mussa Nyamandege amethibitisha kuhairishwa kwa mchezo huo wa ligi baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maji kujaa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid na hivyo kufanya mpira kushindwa kutembea uwanjani.

Mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya Simba dhidi ya TRA United umeahirishwa kutokana na miundombinu ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji kutona na mvua zinazonyesha maeneo mbalimbali ya nchi.

 Akizungumza na Azam TV, Kamishna wa mchezo huo Mussa Nyamandege amethibitisha kuhairishwa kwa mchezo huo wa ligi baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maji kujaa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid na hivyo kufanya mpira kushindwa kutembea uwanjani.

Ameongeza kuwa, mchezo huo uliokuwa umepangwa kuanza saa 10:00 jioni leo utapangiwa siku nyingine na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).