Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF yamjibu Manara

KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesikitishwa na madai ya aliyekuwa mhamasishaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara kuwa alimuomba msamaha kwa maelezo kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia alifanya makosa.

Kidao amesema maneno hayo sio ya kweli, Sekretarieti ya TFF haina nafasi ya kuendelea kuzungumzia jambo ambalo tayari limetolewa uamuzi na chombo huru cha Shirikisho hilo.

Julai 21 mwaka huu Kamati ya maadili ya TFF ilimfungia Manara kujihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili, faini ya Sh. Milion 20 kwa kosa la kumtishia na kumdhalilisha Rais wa TFF.

Manara amefunguka leo akizungumza na waandishi wa habari akipinga hukumu iliyotolewa na TFF akisema haitambui hadi pale atakapopewa barua kuhusu hukumu hiyo na kusema alionekaa akiomba msamaha kwa Karia kwakuwa alitaka kuonyesha umma kuwa mpira ni mchezo wa kiungwana.