Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Mbeya City afichua siri  ya mafanikio

MBEYA CITY Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyewahi kuichezea Ihefu kwa sasa Singida Black Stars na Mbeya Kwanza, alisema jambo lililofanikisha malengo ya timu hiyo kurejea Ligi Kuu Bara ni viongozi wao kufanya usajili bora kulingana na mahitaji waliyoweka.

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, William Thobias amesema haikuwa bahati mbaya kwa timu hiyo kurejea Ligi Kuu, baada ya kushuka msimu wa 2022-2023, kutokana na maandalizi na mikakati bora iliyofanywa na viongozi wa kikosi hicho.

Nyota huyo aliyewahi kuichezea Ihefu kwa sasa Singida Black Stars na Mbeya Kwanza, alisema jambo lililofanikisha malengo ya timu hiyo kurejea Ligi Kuu Bara ni viongozi wao kufanya usajili bora kulingana na mahitaji waliyoweka.

“Ligi ya Championship ni ngumu na ndiyo maana unaposhuka kupanda huwa ni ngumu sana usipokuwa na mikakati mizuri, kwetu ilikuwa rahisi kwa sababu viongozi wote kuanzia wale wa timu na mkoa kiujumla walikuwa wanaongeza lugha moja,” alisema.

Alisema licha ya furaha waliyonayo ya kuirejesha timu hiyo Ligi Kuu ila wana kazi kubwa ya kuendeleza ushindani msimu ujao, kwani kwa sasa hawataki kurudia makosa ya kukishusha kikosi hicho kutokana na ugumu uliopo wa kukipandisha.

Nyota huyo hadi sasa amefunga mabao tisa katika Ligi ya Championship, akizidiwa mawili na mshambuliaji wenzake wa kikosi hicho, Eliud Ambokile anayeongoza na 11, huku kinara ni Andrew Simchimba anayeichezea Geita Gold aliyetupia kambani 18.