Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stamina, Twanga Pepeta wote kunogesha tamasha la biriani

Muktasari:

BENDI ya African Stars 'Twanga Pepeta' na nyota wa miondoko ya taarabu nchini,  Isha Mashauzi 'Jike la Simba' wanatarajiwa kulipamba tamasha la biriani litakalofanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mbali ya Twanga Pepeta na Isha, wengine watakaolinogesha ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya kama Weusi, Baba Levo, Baddest, Dulla Makabila, Stamina na Dj D Ommy atakayeendesha tamasha hilo.

Meneja Biashara na Masoko wa Coca-Cola, Wahida Mbaraka amesema wameandaa tamasha hilo kwa lengo la kuwakutanisha wateja wao na kupata burudani ya pamoja.
Mbaraka amesema maandalizi yake yamekamilika na wameandaa ulinzi mkali kwa ajili ya kuwalinda mashabiki katika tamasha hilo.
Amesema wapishi wa biriani zaidi ya 15 wa Dar es Salaam watakusanyika kwa pamoja katika tamasha hilo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo ya chakula.
Amesema kuwa kampeni ya Biriani Friday na Coke imekuwepo kwa takribani miezi sita sasa ikiwa na malengo ya kuendeleza utamaduni wetu.
Amesema hakutakuwa na kiingilio kwa mashabiki wa burudani ambao wataingia kuanzia saa 4.00 asubuhi mpaka saa 11 jioni na na wale watakaofika baada ya muda huo watalipia Sh 3,000.