Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida yasaka ushindi wa kwanza Kirumba

Muktasari:

  • Timu hiyo imecheza mechi mbili katika Uwanja wa CCM Kirumba na kupoteza zote ikifungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar na bao 1-0 na Azam

KESHO Singida Fountain Gate itacheza mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa ikisaka ushindi wa kwanza itakapoialika Namungo kuanzia saa 10:00 jioni.

Tangu ilipohamishia mechi zake jijini hapa, timu hiyo imeshacheza michezo miwili ya Ligi Kuu na kupoteza yote ikifungwa bao 1-0 na Azam na kuchapwa 2-0 na Mtibwa Sugar, huku ikikamata nafasi ya 12 ikiwa na pointi 21.

Akizungumza leo Machi 15, 2024 jijini hapa, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Ngawina Ngawina amesema baada ya kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Simba wameona mapungufu ya kikosi chao na watayapunguza katika mchezo wa kesho.

Amesema wanaikabili Namungo wakiwa na ujasiri mkubwa kwani wachezaji wote wako salama na wamefanya maandalizi mazuri huku wakiiheshimu Namungo wanayoiheshimu na kutambua ubora wao, hivyo mchezo huo utakuwa na burudani ya kutosha.

“Ni kweli benchi ni jipya tutaendelea kujipanga kesho ni mchezo wetu wa pili tumejiandaa na vijana wako vizuri na tumezungumza nao ili kuwaweka katika hali nzuri naamini katika mechi zijazo tutapata matokeo mazuri,” amesema Ngawina.

“Jambo la muhimu ni watu wa Mwanza watuunge mkono, naamini vijana watafanya kazi nzuri, wachezaji wote wako salama ni machaguzi tu ya kikosi watakaochaguliwa wote watawakilisha vizuri lakini hatuna majeruhi hata mmoja,” amesema.

Nahodha wa timu hiyo, Beno Kakolanya amesema wachezaji wako tayari kufanya kazi na benchi jipya la ufundi na wameliahidi hawatoliangusha kwa sababu nalo limekuja kuisaidia timu hiyo ifikie sehemu inayohitajika.

Amesema japo wachezaji watakuwa na uchovu wa safari kutoka jijini Dar es Salaam lakini siyo kisingizio kwani wote wamejiandaa kwa mchezo wa kesho ambao wanatakiwa kupata ushindi ili kurejesha morali na ubora wao.

“Walimu walichotuambia itabidi tukifuate katika mechi ya kesho ili kupata ushindi, sisi wachezaji tunapaswa kupambana ili kupata matokeo mazuri,” amesema Kakolanya na kuongeza;

"Wachezaji tunachoongea kwa sasa ni kupambana na kuongeza ari, tumekubaliana kutokata tamaa yaliyopita yamekwisha tuangalie mechi zijazo tunazotakiwa kuweka nguvu sana ili tupate matokeo mazuri,” amesema.