Simbu ashindwa kumaliza mbio mashindano ya dunia
Muktasari:
- Simbu alikuwa mwakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano hayo msimu huu.
Wakati Mganda, Victor Kiplangat akitwaa dhahabu, Alphonce Simbu ameshindwa kumaliza mbio ya marathoni kwenye mashindano ya dunia yanayofungwa leo nchini Hungary.
Katika mbio hiyo ya wanaume, hadi kilomita ya 20, Simbu alikuwa kwenye kundi linaloongoza lililotoa bingwa, kabla ya kushindwa kuendelea na kuishia njiani huku akiandika rekodi mpya ya kushindwa kwa na kuishia njiani kwa miaka ya karibuni.
Mganda, Kiplangat aliyetumia saa 2:08:53 alichuana bampa kwa bampa na Muhabeshi, Gabresilase ambaye alichoka kilomita 2 kabla ya kufika kwenye finishing point na kuachwa kwa zaidi ya mita 20 na Kiplangat
Gabresilase alipambana kumfukuza bila mafanikio na kujikuta akikata zaidi 'upepo' hadi kupitwa na Tefeli wa Lesotho aliyetumia saa 2:09:12 na kumaliza wa wa pili, akimuacha kwa sekunde saba Mhabeshi huyo mita chache kabla ya kufika kwenye finishing point.