Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaweka rekodi tatu Kwa Mkapa

BAADA ya kumaliza kipindi cha kwanza cha ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0, dhidi ya Wydad Casablanca, Simba imefanikiwa kuweka rekodi tofauti tofauti.

Kwanza ndio imekuwa timu pekee kutoka Tanzania kumaliza kipindi cha kwanza cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa inaongoza msimu huu kwenye hatua ya makundi.

Vilevile imekuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kwenye michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo wa hatua ya makundi.

Pia kiungo mshambuliaji Andre Onana ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kutoka timu ya Tanzania katika michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza.

Timu nyingine inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kutoka Tanzania ni Yanga, ambayo itacheza kesho na Medeama saa 10:00 kwenye Uwanja wa Mkapa