Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yapigwa faini ya Sh10 milioni waamuzi wafungiwa

Muktasari:

  • Uamuzi huo yalipitishwa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Juni 16, 2026 ambapo Simba, Mtibwa Sugar, Geita Gold, Mapinduzi FC na Moro Kids ni miongoni mwa waliokumbwa na rungu hilo.

KAMATI ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imechukua hatua mbalimbali za kinidhamu dhidi ya klabu, waamuzi, mashabiki na viongozi kufuatia matukio yaliyojitokeza katika michezo ya Ligi Kuu Bara, Championship na First League.

Uamuzi huo yalipitishwa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Juni 16, 2026 ambapo Simba, Mtibwa Sugar, Geita Gold, Mapinduzi FC na Moro Kids ni miongoni mwa waliokumbwa na rungu hilo.

Katika mchezo namba 205 wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kati ya Simba na Pamba Jiji FC, TPLB imeitoza Simba faini ya Sh10 milioni baada ya mashabiki wake kumwagia maji mwamuzi msaidizi namba moja, Frank Komba wakipinga uamuzi yake baada ya kunyoosha kibendera kuashiria mchezaji wa Simba kuotea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tukio hilo ni kosa la kujirudia kwa mashabiki wa Simba ndani ya msimu wa 2025/26 ambapo makosa ya aina hiyo yalijitokeza katika michezo mitatu tofauti na kusababisha klabu kuadhibiwa.

"Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu," sehemu ya taarifa ya Bodi ilieleza.

Katika mchezo huohuo, mwamuzi wa kati Hance Mabena wa Tanga pamoja na Komba wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa michezo mitano baada ya kuonyesha mapungufu yaliyosababisha kushindwa kutafsiri kwa usahihi sheria za soka.

Katika mchezo namba 203 uliochezwa kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar, klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya Sh5 milioni baada ya baadhi ya wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kufanya vitendo vilivyoelezwa kuashirikia imani za kishirikina.

Taarifa ya TPLB imeeleza kuwa baadhi ya wahusika walijikusanya katikati ya uwanja na kuzungumza huku mmoja wa viongozi akionekana akichimba kitu chini katika mchezo huo.

Katika mchezo namba 205 kati ya Mashujaa dhidi ya Yanga, shabiki wa Yanga, Said Selemani Ally, amefungiwa kuingia uwanjani kwa miezi 12.

Kwa mujibu wa TPLB, shabiki huyo aliingia eneo la kuchezea siku moja kabla ya mchezo baada ya Yanga kumaliza mazoezi yake ya mwisho na kumwaga vitu vyenye asili ya kimiminika pamoja na udongo kutoka goli la kusini kuelekea katikati ya uwanja, kitendo kilichotafsiriwa kuwa imani za kishirikina.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 47:2 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Klabu ya Pamba Jiji nayo imepigwa faini ya Sh500,000 baada ya wachezaji wake sita kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba.