Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yapata pigo, Maalim Seif afariki dunia

KLABU ya Simba imepata pigo baada ya kumpoteza mwanachama wake na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki dunia leo saa 5 asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi leo kwenye kituo cha Shirika la Habari Zanzibar (ZBC).
Taarifa ya kuumwa kwake ilitolewa na uongozi wa Chama chake cha ACT Wazalendo, Januari 31 kuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Maalim Seif enzi za uhai wake, alikuwa mwanachama kindakindaki wa Simba akishiriki hadi shughuli za ufunguaji wa matawi ya klabu hiyo na katika mahojiano maalum hivi karibuni na kituo cha luninga cha BBC Swahili, alikiri yeye ni Simba damu na shabiki wa kutupwa wa Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu ya England (EPL).