Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga kazi ipo Kenya

Muktasari:

Vikosi vya timu hizo pamoja na wawakilishi wengine wa Tanzania, JKU kutoka Zanzibar zimeshatua jijini Nairobi ili kwenda kulianzisha Nakuru kunakochezwa michuano hiyo, huku Singida United ikisubiri imalize fainali yake ya Kombe la FA kabla ya kupaa kuwafuata wababe wenzao nchini Kenya.

MZUKA umepanda unaambiwa. Mashabiki wa soka nchini Kenya na ukanda wa Afrika Mashariki wamepata mzuka baada ya kuangalia ratiba ya michuano ya SportPesa Super Cup na kubaini Simba na Yanga zinaweza kuvaana nusu fainali.

Vikosi vya timu hizo pamoja na wawakilishi wengine wa Tanzania, JKU kutoka Zanzibar zimeshatua jijini Nairobi ili kwenda kulianzisha Nakuru kunakochezwa michuano hiyo, huku Singida United ikisubiri imalize fainali yake ya Kombe la FA kabla ya kupaa kuwafuata wababe wenzao nchini Kenya.

Jana Alhamisi vikosi vya Simba na Yanga vilipaa kwenda Kenya tayari kwa michuano hiyo ambapo Yanga itafungua pazia dhidi ya Kakamega Homeboys Jumapili kabla ya watani zao, Simba SC kumenyana na Kariobang Sharks Jumatatu, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Afraha, Nakuru.

Kwa mashabiki wa Yanga habari njema kwao ni straika wao, Ibrahim Ajib ni miongoni mwa wachezaji 20 waliosafiri na kikosi cha timu hiyo kwenda Kenya.

Kikosi kamili cha Yanga kinaundwa na makipa Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, mabeki Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Pato Ngonyani.

Viungo ni Baruan Akilimali, Pius Buswita, Maka Edward, Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Said ‘Ronaldo’ Mussa, Tshishimbi, Yusuf Mhilu na Raphael Daudi, wakati washambuliaji ni Yohana Mkomola, Matheo Anthony na Mrundi Amissi Tambwe.

Wakati huo huo, mabeki Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’, Juma Abdul na straika Obrey Chirwa wamekosekana kwenye msafara huo kutokana na sababu mbalimbali.

BOCCO, OKWI

HAWAPO

Wakati Yanga mambo yakiwa hivyo, kwa Simba imelazimika kuwaacha mastaa wake wawili, John Bocco na Emmanuel Okwi kwenye safari yao ya kwenda nchini Kenya kusaka ubingwa wa michuano hiyo ya SportPesa ambayo bingwa atapewa Dola 30,000 (Sh68 milioni) pamoja na safari ya kwenda nchini England kucheza na Everton.

Kikosi Simba kimesafiri na wachezaji 18, lakini katika orodha hiyo hakuwepo nahodha Bocco ambaye amefunga mabao 14 kwenye msimu uliomalizika, pamoja na mfungaji bora wa Ligi Kuu, Okwi.

Nyota wengine watatu wa kikosi cha kwanza ambao hawapo katika orodha hiyo ni Waghana Nicholas Gyan, Asante Kwasi na James Kotei. Wengine ni Juma Liuzio, Salim Mbonde, Laudit Mavugo, Emmanuel Mseja, Jamal Mwambeleko, Kelvin Faru na Vincent Costa.

Katika orodha ya waliosafiri straika mpya wa Simba, Marcel Kaheza aliyefunga mabao 14, akiwa na kikosi cha Majimaji kilichoshuka daraja kabla ya kutua Simba naye amejumuishwa.

Wachezaji waliosafiri Aishi Manula, Said Mohamed, Ally Salim, Ally Shomary, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Yusufu Mlipili, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Muzamir Yassin, Moses Kitandu, Rashid Juma, Said Ndemla, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya na Mohamed Ibrahim ‘MO.