Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yakiri kosa, kuilipa Teungueth

Uongozi wa klabu ya Simba umekiri hakukuwa na mawasiliano na klabu ya Teungueth ya nchini Senegal iliyoshinda kesi ya madai kuhusu dili la Pape Sakho kwenda Ufaransa.

Mchana leo ilitoka taarifa ya FIFA kuifungia Simba kusajili hadi iilipe klabu ya Teungueth sehemu ya mauzo ya Sakho kutoka Simba kwenda Quevilly Rouen Metropole ya Ufaransa ambapo Simba imeeleza kupitia taarifa yao kuwa ilikuwa ikisubiri malipo ya awamu ya pili.

"Malipo ya awamu ya kwanza asilimia 50 yalilipwa Oktoba 2, 2023, klabu ya Simba ilikuwa inasubiri awamu ya pili ili kulipa asilimia 15 ya mauzo kwa klabu ya Teungueth ya Senegal,"

"Klabu ya Simba inakiri kulikuwa hakuna mawasiliano ya Teungueth ya Senegal yaliyopelekea kadhia hii. Hata hivyo Simba inapenda kuujulisha umma kuwa iko mbioni kukamilisha malipo hayo hivi punde," imeeleza taarifa ya Simba