Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yafungiwa kusajili

Shirikisho la Soka la kimataifa (FIFA) limeifungia kusajili Simba SC hadi ilipe madai ya klabu ya Teungueth ya Senagal kuhusu dili la mchezaji Pape Sakho.

Barua ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) imeeleza uamuzi huo uliofanywa na FIFA umetokana na Teungueth kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho ambaye kwasasa anachezea Union Sportive Quevillaise-Rouen Métropole ya nchini Ufaransa.

"Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya Sakho. Simba ilitakiwa iwe imetekeleza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa, lakini haikufanya hivyo,"

TFF imeeleza wakati FIFA ikiifungia Simba kufanya uhamisho wa wachezaji wa kimataifa, wao wameifungia kufanya uhamisho wa ndani.