Simba waweka kikosi kizima kuwavaa Yanga

KOCHA mkuu wa Simba Didier Gomes tayari ameweka wazi kikosi cha kwanza kitakachocheza mechi ya fainali kombe la Azam dhidi ya Yanga muda mchache ujao na kujaza mastaa wote ndani.
Gomes hajapangua kitu kwenye safu ya ulinzi akimuanzisha kipa Aishi Manula na mabeki Mohammed Hussein, Shomari Kapombe, Joash Onyango na Pascal Wawa.
Viungo Gomes ameanza na wanne, Taddeo Lwanga, Rally Bwalya, Clatous Chama na Luis Miqquisone.
Katika eneo la ushambuliaji, Simba itaanza na washambulisji wawili, John Bocco na Chris Mugalu wakitumia mfumo wa 4-4-2.
Wachezaji waliopo benchi ni Beno Kakolanya, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, Bernard Morrison, Hassan Dilunhga na Meddie Kagere.
Mchezo huo unaowakutanisha watani hao wa jadi utaanza saa 10:00 jioni kwenye dimba la Lake Tanganyika, Kigoma.