Shabiki wa Simba alamba Sh49 milioni
SIMBA imeshinda leo kule Kaitaba kwa mabao 5-2 dhidi ya Kagera Sugar lakini kuna shabiki yao mmoja naye ametusua mapesa akishinda zaidi ya Sh49 milioni.
Haji Mussa ambaye ni mfanyabiasha mdogomdogo maarufu machinga na shabiki wa Simba ameshinda fedha hizo kupitia mchezo wa kubahatisha ya kampuni ya Premier Bet kupitia tiketi ya 'Book Maker' akitumia mechi sita tu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya fedha hizo Meneja Rasilimali wa kampuni hiyo, Amanda Kusila amesema wamefarijika kuzalisha milionea huyo wakati huu mwaka 2024 ukielekea ukingoni.
"Tunao washindi wengi ndani ya mwezi huu ambao wamejishindia jumla ya Sh30 milioni lakini huyu Haji Mussa ni ushindi mkubwa kwa kushinda wote hao, hii ni hatua kubwa kwa wale ambao wameamua kubashiri kistaarabu," amesema Kusila.
Naye Mussa amesema amewahi kushinda fedha lakini ushindi huu wa sasa ni mkubwa zaidi ambapo anataka kuzitumia kutanua biashara zake.
"Nimekuwa nashinda kiasi mbalimbali lakini sio kwa kiwango hiki, unajua mimi ni mmachinga hizi fedha nakwenda kutanua biashara zangu ili nijiongeze kibiashara," amesema Mussa.
Ushindi wa Mussa umeenda sambamba na ushindi wa timu yake ya Simba ambayo iliupata kule Kaitaba na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.