Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Girls, Uganda kupigania taji la CECAFA U-17

Muktasari:

  • Serengeti Girls ilionyesha ubora wake mbele ya mashabiki wa nyumbani baada ya kuichapa Sudan Kusini mabao 4-0 na kutinga fainali kwa kishindo. Fainali itapigwa Julai 23 Uwanja wa KMC Complex.

SAFARI ya kutafuta bingwa wa CECAFA U-17 kwa Wanawake 2026 imeendelea leo jioni baada ya wenyeji Tanzania 'Serengeti Girls' na mabingwa watetezi Uganda kufuzu fainali ya michuano hiyo kufuatia ushindi mnono walioupata katika michezo ya nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Serengeti Girls ilionyesha ubora wake mbele ya mashabiki wa nyumbani baada ya kuichapa Sudan Kusini mabao 4-0 na kutinga fainali kwa kishindo. Fainali itapigwa Julai 23 Uwanja wa KMC Complex.

Mabao katika mechi hiyo yalifungwa na Bahati Kizanguzi aliibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili, huku Harrier Juma na Yasinta Kaluwa kila mmoja akifunga moja na kuihakikishia Tanzania kufuzu hatua hiyo.

Upande wa Uganda baada ya kuifunga Kenya mabao 3-0 katika nusu fainali nyingine iliyopigwa mapema uwanjani hapo.


SAFARI YA SERENGETI GIRLS

Tanzania imeingia hatua hiyo ikiwa na rekodi nzuri baada ya kumaliza Kundi A kileleni kwa pointi saba, ikifunga mabao 15 na kuruhusu bao moja pekee. Kikosi hicho kimeonyesha ushindani mkubwa hasa kwenye safu ya ushambuliaji na uimara wa safu ya ulinzi, hali inayokifanya kuwa miongoni mwa timu zinazotajwa kuwania taji hilo.

Ushindi wa mabao 4-0 katika nusu fainali umeifanya Tanzania kufikisha idadi ya mabao mengi katika mashindano hayo huku ikionyesha uimara mkubwa safu ya ushambuliaji na ulinzi.

Safari ya Uganda kwenye michuano hiyo imekuwa timu ya kutisha zaidi hadi sasa baada ya kushinda mechi zote tatu za kundi, ikifunga mabao 20 na kutoruhusu hata bao moja. Takwimu hizo zinaifanya Teen Cranes kuingia nusu fainali ikiwa miongoni mwa timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.