Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sanchez majanga huko Man United

Muktasari:

Hali ngumu ndani ya kikosi cha Manchester United kutokana na madai kuwa Alexis Sanchez anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.

MANCHESTER, ENGLAND
HABARI ndiyo hiyo. Manchester United inaweza kuikosa huduma ya staa wao Alexis Sanchez kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja na hivyo kuwa pigo kubwa katika mechi zao za kibabe zinazowakabili ndani ya mwezi huu.
Mwandishi wa habari mmoja mwenye uhusiano mzuri sana na Man United, Duncan Castles alisema staa huyo wa kimataifa wa Chile ameumia na hivyo atakuwa nje ya uwanja pengine inaweza kuwa kwa mwezi mzima, ikiwa ni kipindi muhimu sana kwa timu hiyo kuwa na huduma ya mchezaji huyo kwenye Ligi Kuu England.
Hata hivyo, kumekuwa na taarifa nyingine zinazodai mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili.
Kama lisemwalo lipo na kisha Sanchez akawa nje ya uwanja kwa mwezi mzima, basi jambo hilo litamfanya akose mechi nane, ikiwamo dhidi ya Arsenal, timu yake ya zamani na Liverpool uwanjani Anfield. Mechi nyingine kubwa atakayokosa ni ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya kukamilisha hatua ya makundi dhidi ya Valencia.
Hata hivyo, jambo hilo limekuwa pigo hata kwa Sanchez mwenyewe ambaye alitaka kutumia mwezi huu wa Desemba kuonyesha kiwango bora kabisa ili kuzivutia timu nyingine hususani Paris Saint-Germain ili kuja kumsajili dirisha la Januari. Kama Sanchez atakuwa kweli mgonjwa na kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima, hii ndio orodha ya mechi atakazokosa.
Southampton – ugenini (Desemba 1)
Arsenal – nyumbani (Desemba 5)
Fulham – nyumbani (Desemba 8)
Valencia – ugenini (Desemba 12)
Liverpool – ugenini (Desemba 16)
Cardiff – ugenini (Desemba 22)
Huddersfield – nyumbani (Desemba 26)
Bournemouth – nyumbani (Desemba 30)