Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samson Mbangula kukosa mecho zote Ligi Kuu

Mbangula Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo ambaye msimu uliopita aliifunga Simba mabao mawili katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambao ulimalizika kwa Prisons kushinda 2-1.

STRAIKA tegemeo wa Tanzania Prisons, Samson Mbangula atakosa mechi zote zilizobaki msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, Jumatatu wiki hii, katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Dar es Salaam.

Mchezaji huyo ambaye msimu uliopita aliifunga Simba mabao mawili katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambao ulimalizika kwa Prisons kushinda 2-1.

Mara ya mwisho kwa mchezaji huyo kuonekana uwanjani katika kikosi hicho ilikuwa Oktoba 26, 2024 wakati timu yake ilipofungwa mabao 2-1 na KMC katika Uwanja wa Sokoine - Mbeya na baada ya hapo hajacheza tena kutokana na maumivu ya goti la kulia.

Kutokana na ukubwa wa majeraha hayo, nyota huyo wa Tanzania Prisons amelazimika kufanyiwa upasuaji huo ambao utamfanya arejee uwanjani, Julai mwaka huu.

“Sikuwa katika hali nzuri na kadri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda mbele, maumivu yakawa yanazidi kuongezeka na nikawa napata tabu hata kutembea ndio nikaona nifanye vipimo ambapo madaktari wakanishauri kwamba nahitajika kufanyiwa upasuaji.

“Namshukuru Mungu upasuaji umefanyika vizuri na sasa ndio hivi najiuguza. Kwa mujibu wa maelezo ya madaktari, nitahitaji kama miezi sita hivi kupona na hapo ndio nitarejea uwanjani,” alisema Mbangula.

Upasuaji wa Mbangula umefanyika katika kipindi ambacho Tanzania Prisons inamkosa mshambuliaji mwingine tegemeo wa kikosi cha kwanza, Jeremiah Juma ambaye naye ni majeruhi.

Hapana shaka kwa sasa kocha Amani Josiah atawategemea Yusuph Athuman, Kelvin Sabato na Adam Adam ambao wamesajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Yusuph amenaswa akitokea Fountan Gate, Adam anatoka Azam FC na Sabato amesajiliwa kutokea Singida Black Stars.