Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta ampigia kura Van Dijk, Ndayiragije kwa Messi

Muktasari:

Samatta atakutana na Van Dijk aliyempigia kura ya kuwa mchezaji bora wa dunia pamoja na Mane kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Oktoba 23 ambapo KRC Genk itaanza kwa kuikaribisha Liverpool kabla ya kurudiana Anfield.

Dar es Salaam. Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta alimpigia kura beki wa Liverpool, Van Dijk Virgil, Kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije yeye alimpigia kura Lionel Messi katika tuzo za mchezaji bora wa dunia wa mwaka Fifa.

Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel  Messi  wa FC Barcelona hawakuwa kati ya wachezaji watatu ambao Samatta aliwachanganua na kuona wanafaa  kwa kuwapigia kura  kuwa wachezaji bora kwa mwaka huu, 2019.

Hata hivyo, kura ya Samatta haikutosha kumfanya beki wa Liverpool kuwa mchezaji bora wa dunia, ambapo kwenye usiku wa jana kwenye jiji la Milan, alitangazwa Messi kutwaa tuzo hiyo kwa mara sita huku beki huyo wa Kiholanzi akishika nafasi ya pili.

Mbappe na Mane walipata kura za Samatta katika nafasi ya pili na tatu, hawakuweza kupenya kwa kuingia hata kwenye tatu bora ya wachezaji bora wa dunia.

Kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije  chaguo lake la  kwanza lilikuwa Messi, akafuata Cristiano Ronaldo  huku Mohamed Salah akiwa katika nafasi ya tatu.

Upande wa nahodha na kocha wa Uganda, Denis  Onyango anayeichezea Mamelodi Sundowns F.C. , aliwachagua, Van Dijk, Salah na De Jong huku Abdallah  Mubiru  kwake ikiwa, Mbappé , Ronaldo na  Messi

Kura ya Kenya, ilipigwa na mwandishi wa habari pekee, Toskin Robin kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, ambayo alielekeza kwa  Van Dijk, Ronaldo na  Salah.