Sahara Power kutumia baskeli kupambana na hewa chafu ya kaboni

Kampuni ya Sahara Power Group inayofanya kazi ya kuzalisha umeme,  imeamua kupambana na kupunguza hewa chafu ya kaboni kwa kuhamasisha matumizi ya kuendesha baiskeli kwenye miradi ya umeme na utunzaji wa mazingira iliyopo Egbin.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), linaeleza kutembea na kuendesha baiskeli inapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, kiharusi, kansa, kisukari na vifo.
Akizungumza kwenye Siku ya Baiskeli Duniani (inayofanyika Juni 3) iliyofanyika Egbin Lagos nchini Nigeria, Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Power, Kola Adesina amesema kuzingatia utunzaji wa mazingira duniani,  husaidia uendeshaji mzuri wa baiskeli kwenye maeneo yao yakiwemo ya Egbin, Ikeja Electric na First Independent Power Limited.
Adesina amesema Egbin imejijengea utamaduni huo baada ya kuwapa baiskeli 150 wafanyakazi wake kuhamasisha usafi, afya na uzalishaji ambao umesaidia kuhifadhi lita trilioni za maji safi.
Sahara Power imepanga kuagiza baiskeli 500 kwa ajili ya kampeni ya mazingira, kupanda miti, wafanyakazi kutembea na kufanya mazoezi inayofanyika kwa mwezi na shughuli nyingine zinazokutanisha wadau mbalimbali.
Egbin imesherehekea siku hiyo kwa matukio yaliyohusisha mtu mmoja mmoja na makundi kwa kuendesha baiskeli kuzunguza eneo la mradi na sehemu za shule ili kuipatia hamasa jamii ya kuanza kutumia baiskeli kwenye safari zao mbalimbali.
“Baiskeli imekuwa sehemu ya maisha hapa Egbin, tumeona matokeo yake kwenye uzalishaji na utendaji. Tutaendelea kusaidia kampeni za kidunia kuhusu utunzaji wa mazingira ili kuifanya dunia kuwa safi na yenye afya salama,” alisema Adesina.