Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu za Azam FC, Mtibwa Sugar kujiondoa michuano ya vijana U20 wilaya ya Morogoro 2022

Baadhi ya sehemu ya mashabiki wa soka wakifuatilia michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 wilaya ya Morogoro 2022 inayoendelea kuchezwa katika uwanja wa Sabasaba mkoani hapa. Picha na Juma Mtanda

Morogoro. Kujiondoa kwa timu za soka za vijana za Azam FC na Mtibwa Sugar kwa kumeshindwa kushiriki michuano ya vijana ya umri wa miaka 20 (U20) wilaya ya Morogoro 2022 kumepelekea kupunguza mvuto wa michuano hiyo kufuatia hapo awali timu hizo kudhibitisha kushiriki katika michezo hiyo mkoani hapa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti mjini hapa, Katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Morogoro (MDFA), Geofrey Mwatesa alisema michuano hiyo ilipanga kushirikisha jumla ya timu 23 na kati ya timu hizo nne zimealikwa kunogesha mashindano hayo ikiwemo ya Azam Fc na Mtibwa Sugar na huenda kwa timu hiyo kumepunguza msisimko.

Mwatesa alisema miongoni mwa timu alikwa ni pamoja na Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar, Kilombero Soccer Net na Azam U20 lakini wakati mashindano yanakaribia kuanza walipokea taarifa kutoka kwa viongozi wa timu ya Mtibwa Sugar na Azam Fc kuwa hawataweza kushiriki kutokana na sababu mbalimbali.

“Michuano hii tulipanga kushirikisha jumla ya timu 23 kati yao ni timu alikwa zikiwemo Azam Fc U20 na Mtibwa Sugar lakini viongozi wa timu hizo wameleta taarifa kuwa hawataweza kushiriki kwa sababu mbalimbali na tumebakiwa na timu 21 hivyo timu alikwa kwa sasa ni Ruvu Shooting, Kilombero Soccer Net na Pwani Sports Foundation na zilizobakia zikitokea hapa Manispaa.”alisema Mwatesa.
Mwatesa alisema upande wa Azam Fc U20 wameshindwa kushiriki kwa sababu mashindano haya yatachukua muda mrefu wa mwezi moja huenda hilo ikawa moja ya chanzo cha wao kushindwa kushiriki michuano hiyo.
Kwa upande wa Meneja wa timu ya Mtibwa Sugar, David Bugoya alisema moja ya sababu ya wao kujiondoa katika michuano ya U20 wilaya ya Morogoro 2022 hawakufanya maandalizi mapema kuelekea michuano hiyo.

Bugoya alisema kwa sasa uongozi wa Mtibwa Sugar unaelekeza nguvu zaidi katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara ya NBC kwa ajili ya kujikita zaidi katika maandalizi ya timu hiyo katika msimamo kutokana na kutokuwa katika nafasi nzuri.

“Tumejiondoa mashindano ya vijana ya U20 ya wilaya ya Morogoro kwa timu ya vijana ya Mtibwa Sugar na kushindwa kwetu kushiriki kwa sababu tumechelewa kufanya maandalizi na tumeona tuelekeze nguvu kubwa yetu ya timu katika michezo ya ligi kuu ya NBC iliyobakia kwa sababu hatuko katika msimamo nzuri zaidi.”alisema Bugoya.

Mtibwa Sugar katika msimamo wa ligi ipo nafasi ya 11 ikiwa imekusanya alama 23 baada ya kushuka uwanjani mara 20 huku Mbeya Kwanza ikiburuza mkia kwa kukusanya alama 18 katika michezo 21 iliyocheza.