Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo alilala kitandani na mpira-5

Muktasari:

  • Jorge amewahi kusikia matukio ya watoto ambao wazazi wao walijifungua kwa kutumia mikasi hiyo ambao wamesababisha madhara kwa watoto ikiwamo kuwa na matatizo ya akili.

TOLEO lililopita mwandishi, Luca Caioli aligusia mazingira yalivyokuwa wakati Messi na Ronaldo wanazaliwa jinsi ujauzito wa Messi ulivyoibua hofu kwa baba yake na jinsi mimba ya Ronaldo ilivyoishangaza familia hiyo ambayo haikutarajia kupata mtoto mwingine. Endelea…

Jorge amewahi kusikia matukio ya watoto ambao wazazi wao walijifungua kwa kutumia mikasi hiyo ambao wamesababisha madhara kwa watoto ikiwamo kuwa na matatizo ya akili.

Ni kama maombi yake yalisikika, mwishowe, Dk Odetto akamwambia kwamba mikasi hiyo isingetumika na hatimaye Juni 24. 1987, dakika kadhaa baada ya saa 12 asubuhi, mtoto Lionel Andres Messi anazaliwa.

Hofu yote ikatoweka, familia ikawa na kila sababu ya kufurahia, mtoto huyo mpya (Messi) mwenye kilo tatu pia alikuwa mwenye afya.

Leo amekulia katika nyumba ambayo Jorge (baba yake) alikuwa akiijenga kila siku za mwisho wa wiki akisaidiana na baba yake Eusebio, ni nyumba ya matofali katika kiwanja cha mita za mraba 300, kwa nyuma ikiwa na eneo ambalo wato walikuwa wakilitumia kwa ajili ya kucheza.

Ni nyumba ambayo iko katika mitaa ya Las Heras karibu na Rosario kwa upande wa kusini, wenyeji wa maeneo hayo ni watu wastaarabu na wahangaikaji wenye bidii.

Jorge ni kiongozi wa idara katika kampuni inatotengeneza bidhaa za bati wakati mkewe Celia anafanya kazi katika karakana inayotengeneza vifaa vya umeme.

Huko Madeira baba mzazi wa Cristiano Dinis ni mtayarishaji na msimamizi wa bustani wakati mkewe Dolores alikuwa akipika chakula na kuuza pamoja na kuweka mazingira sawa kwa ajili ya chakula cha familia.

Kama ilivyo kwa wananchi walio wengi wa Ureno, Dolores naye akiwa na miaka 20 alihamia Ufaransa na kufanya kazi ya kusafisha nyumba kwa miezi mitatu.

Mumewe naye alikuwa mbioni kuungana naye lakini aliposhindwa kufanya hivyo, Dolores naye akaamua kurudi nyumbani Madeira. Tayari walikuwa na watoto wawili na maisha kwa upande wao hayakuwa rahisi.

Ni magumu hivyo hivyo kwa yeyote ambaye anaishi mbali na mji ulioendelea wenye uwekezaji katika mahoteli ambayo yalitawala eneo lote la Pwani.

Walikuwa wakiishi nyumba ndogo ya familia ya watu sita, nyumba ambayo likitokea kumbunga kidogo tu inapata nyufa kila kona, Dolores alikuwa akitafuta vipande vya mawe na saruji katika majengo makubwa ya mjini kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.

Hata hivyo pamoja na hali yote hiyo, Cristiano Ronaldo leo hii bado anayakumbuka maisha yake ya utotoni na kuyataja kuwa ni yaliyojaa furaha, akiwa na miaka miwili au mitatu alikuwa akicheza kwenye eneo la wazi au mtaani, taratibu alianza kumbaini rafiki yake mkubwa ambaye ni soka.

“Kuna siku moja wakati wa Krismasi nilimpa gari inayoendeshwa kwa ‘remote’ nilidhani ingemshughulisha, anakumbuka mmoja wa walezi wake, Fernao Sousa na kufafanua kwamba alichopenda Ronaldo ni kucheza soka tu.

“Hata kitandani alilala akiwa na mpira, hakuwahi kuuweka kando, wakati wote mpira ulikuwa mkononi mwake popote alipokwenda alikuwa na mpira.”

Mapenzi ya Ronaldo katika soka yalikuwa na mkono wa familia, baba yake alikuwa msimamizi wa vifaa katika klabu ya mtaani ya Andorinha na haikushangaza nahodha wa timu hiyo kuwa Sousa, mmoja wa walezi wa Ronaldo.

Dinis na Sousa inadaiwa waliwahi kuchelewa kwenye hafla ya ubatizo kwa sababu hawakutaka kuikosa mechi ya Andorinha dhidi ya Ribeira Brava.

Itaendelea Jumamosi ijayo…