Rhino, Toto, Pamba kumaliza kweupe

Muktasari:
Timu zote zimebakiza mechi mbili katika Kundi C linaloongozwa na Biashara United ya mkoani Mara yenye pointi 24, ikifuatiwa na Alliance (22) sawa na Dodoma, Rhino (15),Oljoro na Trans Camp (zote 14), Pamba 12 na Toto pointi 10.
Mwanza. Wakati Ligi Daraja la kwanza ikielekea ukingoni, hatma ya timu za Mwanza,Toto Africans na Pamba kubaki katika ligi hiyo imeshikiriwa na Rhino Rangers. katika Kundi C.
Timu zote zimebakiza mechi mbili katika Kundi C linaloongozwa na Biashara United ya mkoani Mara yenye pointi 24, ikifuatiwa na Alliance (22) sawa na Dodoma, Rhino (15),Oljoro na Trans Camp (zote 14), Pamba 12 na Toto pointi 10.
Rhino ya Tabora imeshikiria hatma ya Pamba na Toto kwani mechi zilizobaki kwa wajeda hao ni kukutana na timu hizo kuwa katika hali mbaya kushuka daraja.
Toto itaanza kuwafuata wapinzani hao mkoani Tabora kujiuliza kama watapata huruma ili waweze kupumua, ili mechi yao ya mwisho dhidi ya Dodoma wacheze kupata ushindi au sare.
Pia, Pamba iliyo nafasi ya saba kwa pointi 12, iwapo watapoteza mchezo wao ujao dhidi ya Alliance FC, basi watapaswa kuwapigia magoti Rhino ili washinde waepuke na dhahama ya kushuka daraja.
Hata hivyo, wakati timu hizo zikiomba matokeo mazuri kwenye mechi hizo, bado zinaombeana mabaya ili mmoja wapo apoteze ili mwingine aweze kusalia kwenye Ligi Daraja la kwanza.
Rhino nao hawako salama kwa asilimia zote, kwani pointi zao 15 hazitoshi kutamba kubaki kwenye Ligi, kwani Oljoro naTrans Camp wenye alama 14 sambamba na timu hizo za Mwanza kama zitashinda mechi zote,Rhino wanaweza kushuka Daraja.
Mechi za Rhino ni kama kipimo kwao, kwani kama watamruhusu Toto kupita, basi wanapaswa kumnyonga Pamba mechi yao ya mwisho ili wajihakikishie kubaki katika ligi hiyo.