Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pondamali aiweka Yanga pembeni kwa Singeli

Muktasari:

  • Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali amekuwa akiifundisha timu hiyo kwa kipindi kirefu. Pia ni klabu ambayo alikuwa akiichezea hapo awali.


HIVI sasa ukitaka kumtafuta kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali yupo studio anaandaa nyimbo zake za Singeli na muda wowote ataachia wimbo wake wa Pesa Baba Yake Nani na mambo ya soka ameweka pembeni.
Pondamali ambaye anawanoa makipa wa Yanga kwa kipindi kirefu na sasa eneo lake limeboreshwa baada ya kusajiliwa mawili Mkenya Farouk Shikalo na Metacha Mnata ambao wataungana na Ramadhani Kabwili pamoja na Mkongo Klaus Kindoki.
Hata hivyo, kuna habari kwamba Kindoki huenda wakaachana naye na kumlipa masilahi yake ya kimkataba kwani bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Desemba.
Amesema, ameamua kujikita studio kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake kwani ndio kipindi pekee ambacho anaona ana muda wa kufanya hivyo.
"Ligi ikianza mambo yanakuwa mengi unakuwa bize na mpira tu kusafiri sana, ukiwa kwenye ligi unatakiwa akili ikitulie katika kupanga programu na mambo mengine,"alisema Pondamali.
"Nimeingia studio naandaa wimbo wangu mpya unaitwa Pesa Baba Yake Nani, uko kwenye hatua za mwisho ndani ya siku mbili hizi utakuwa tayari tutaiachia."
Hata hivyo, hakutaka kuzungumzia sana usajili wa makipa hao ndani ya kikosi cha Yanga na kusema ni mipango ya timu akitulia atafanyia kazi.