Polisi Tanzania: Hatufuati pesa mechi ya Simba

BAADA ya Polisi Tanzania kuhamishia mechi yao dhidi ya Simba katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa hawafuati pesa jijini humo bali ni kubadilisha tu mazingira.
Katika mechi 30 za Ligi Kuu Bara ambazo Polisi Tanzania imecheza hadi sasa mechi zake 14 za nyumbani imecheza viwanja vinne vya mikoa mitatu ambazo ni Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro dhidi ya JKT Tanzania, Dodoma Jiji, Ruvu Shooting, Azam FC, Mbeya City, Tanzania Prisons na Namungo.
Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mechi dhidi ya Gwambina, Biashara United, Yanga na KMC, Azam Complex Dar dhidi ya Ihefu FC na Uwanja wa Uhuru pia Dar dhidi ya Mtibwa na Coastal Union ambapo mechi hizo imeshinda nne sawa na michezo iliyopoteza sare 6 na kuambulia pointi 18 pekee kati ya 42 na huku ikipoteza pointi 24.
Michezo 16 ya ugenini imeshinda mitano, sare nane na kupoteza mitatu huku ikikusanya alama 23 na kupoteza 25 kati ya 48. Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo Robert Munisi, alisema kuwa;
“Suala la pesa? Kwani mechi ya Simba najua nitapata shilingi ngapi? Hatuendeshi timu kwa kutegemea viingilio, tuna wafadhili bado kuna hela za bodi kuna sababu nyingi.”