Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi, KMC zatunishiana misuli

Polisi, KMC zatunishiana misuli

Timu za Polisi Tanzania na KMC zimeonyesha kila mmoja kuwa na njaa ya pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu NBC unaotarajiwa kuchezwa kesho saa 10:00 jioni katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Wakizungumzia na maandalizi ya mchezo huo makocha kutoka pande zote wametamba kuibuka na ushindi dhidi ya mwenzake.

Kocha msaidizi wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema kuwa wamefanikiwa kuongezeka wachezaji wanne ambao walikosekana kwenye mchezo wa awali wa ligi dhidi ya Yanga, hali wanayoamini kikosi kimeimarika kwa ajili ya mchezo huo.
Polisi inashuka dimbani kuivaa KMC kwa Ari kubwa huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Yanga kwa mabao 2-1.
"Tuliumia na matokeo ya mchezo wa awali lakini hii ilisababishwa na baadhi ya wachezaji wetu tegemezi walikuwa majeruhi na wale wa kigeni kutokupata vibali lakini namshukuru Mungu kesho idadi ya sura ngeni itaongezeka kati ya wale tegemeo wetu wamerudi katika Hali zao." alisema Tamba.

Kwa upande wake nahodha wa timu ya Polisi Tanzania, Tariq Simba amesema kuwa wachezaji wenzake wana morali ya hali ya juu kuivaa KMC kuhakikisha wanavuna ushindi na kuwataka mashabiki wao wategemee furaha kesho.

"Kupoteza mchezo wa awali tuliumia sana, lakini tumefanikiwa kujipa moyo na kufanya maboresho makubwa namshukuru Mungu hadi jana tulifanya mazoezi wachezaji wengi wamerudi katika hali za kawaida na tunawaahidi ushindi." alisema Simba.

Kwa upande wake kocha wa KMC, Ahmed Ally alisema wamejiandaa kuhakikisha wanavuna pointi tatu dhidi ya Polisi katika mchezo wa kesho ili kuondoa uteja wa viwanja vya kaskazini.

"Mchezo wetu utakuwa mgumu ukizingatia wapinzani wetu nao walifungwa mechi ya awali kama sisi hivyo kila mmoja anataka matokeo, lakini kwa upande wetu nadhani sisi tunahitaji alama tatu zaidi kwa sababu ya kulipiza kisasi lakini kuvunja rekodi ya kufungwa kila tunapokuja Arusha." alisema kocha Ally.

Kocha huyo alisema kuwa mechi ya awali ya Polisi dhidi ya Yanga waliitazama vizuri na wamewajua wapinzani wao vema hasa ubora wa kikosi na pumzi kubwa waliyonayo hivyo wataingia na tahadhari kubwa ya kuwaheshimu na kuusoma mchezo.

KMC wanaingia tena dimbani ugenini katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha kuivaa Polisi wakiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

"Polisi tunajua ni wazuri maana mchezo wao wa awali tuliutazama vema na tukauona ubora wao lakini na sisi naamini wametuona hivyo tunaingia tukijuana lakini mapungufu yetu tumeyafanyia kazi na tunaamini tutaibuka na Ushindi kupunguza machungu ya mchezo wa awali hivyo mashabiki wetu wanaweza kutegemea furaha." alisema kocha Ally.

Nae nahodha wa timu ya KMC, Mohamed Samatta alisema kuwa kumbukumbu ya kufungwa mchezo wa awali hauwatoi kwenye matumaini ya kuchukua pointi tatu kesho dhidi ya Polisi.

"Tumefuata alama tatu, kupoteza mchezo wa awali haitoi hatma yetu ya kesho kwani maboresho makubwa yamefanyika na tutaenda kuonyesha kazi kesho uwanjani." alisema Samatta.