Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba apunguza mshahara kutua Real Madrid

Muktasari:

  • Man United wanataka kumbakiza Pogba kwenye kikosi chao, lakini baada ya mambo kwenda hovyo huko Old Trafford na kukosekana kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa haonekani kama atakubali kubaki kwenye kikosi hicho

MADRID, HISPANIA. PAUL Pogba amepania. Kisemwacho ni kwamba mpango wa kiungo huyo ni kwenda Real Madrid na kwamba atashusha mshahara wake kwa Pauni 3 milioni ili kufanisha dili hilo la kuhama Old Trafford kwenda kukipiga Bernabeu.

Taarifa zaidi zinasema kwamba Pogba kwenda Madrid ni jambo linalosubiri tu wakati kufika huku ikielezwa amekubali kupunguza mshahara wake kwa Pauni 3 milioni kwa mwaka ili kukamilisha uhamisho huo ambao utagharimu Pauni 150 milioni.

Eden Hazard akiwa tayari kwenye mpango wa Real Madrid na kuwa mmoja wa usajili moto kwenye kikosi hicho cha Los Blancos,  Pogba anataka kwenda kuungana na fundi huyo wa mpira wa Kibelgiji huku ikiripotiwa kwamba Adidas watafanikisha dili hilo.

Kipindi kimoja cha soka cha kila wiki cha El Chiringuito de Jugones, kilifichua kwamba mwandishi maarufu wa huko Hispania, Eduardo Inda amedai kwamba: "Pogba dili lake ni kama limeshakamilika.

"Usajili wa kwanza utakuwa wa Hazard na unaofuatia ni wa Pogba. Amekubali kupunguza mshahara wake anaolipwa huko Manchester United, kutoka Pauni 13 milioni kwa mwaka hadi Pauni 10 milioni.

"Nadhani Madrid watamchukua kwa ada ya kati ya Pauni 137 milioni na Pauni 150 milioni. Adidas wanapambana sana kufanikisha dili hilo kwa sababu yeye ni moja kati ya wachezaji wawili wenye brandi kubwa."

Man United wanataka kumbakiza Pogba kwenye kikosi chao, lakini baada ya mambo kwenda hovyo huko Old Trafford na kukosekana kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa haonekani kama atakubali kubaki kwenye kikosi hicho.

Kocha Ole Gunnar Solskjaer atakuwa mwenye furaha Pogba akiondoka, licha ya kwamba mabosi wake hawataki hilo litokee kwa sababu za kibiashara.