Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pandya arudi mbio za magari

PANDYA Pict

Muktasari:

  • Yakijulikana kama Mkwawa Rally of Iringa, mashindano haya ya siku mbili yatachezwa mkoani Iringa Mei 24 na 25 mwaka huu yakishirikisha madereva kutoka ndani na nje ya Tanzania, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Mbio za Magari Iringa, Robert Maneno.

BINGWA wa zamani wa mbio za magari nchini, Dharam Pandya ametangaza rasmi kurudi mchezoni na atakuwa mmoja wa washiriki katika mbio za ufunguzi wa msimu mkoani Iringa mwishoni mwa juma.

Yakijulikana kama Mkwawa Rally of Iringa, mashindano haya ya siku mbili yatachezwa mkoani Iringa Mei 24 na 25 mwaka huu yakishirikisha madereva kutoka ndani na nje ya Tanzania, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Mbio za Magari Iringa, Robert Maneno.

“Narudi kushika usukani tena baada ya kupumzika kwa miaka michache. Subaru Impreza ikiwa katika ubora ule ule, ndiyo mashine ya ushindi mwaka huu,” alisema Dharam Pandya.

Pandya anarudi kwenye mbio za magari akikuta mchezo huo unashikiliwa na Manveer Birdi ambaye ndiye dereva bora  wa mwaka 2024 na anarudi Iringa kama bingwa mtetezi wa mbio za magari za Mkwawa baada ushindi wake wa mwaka jana.

Kwa mujibu wa orodha ya washiriki iliyotolewa na waandaaji, klabu ya mbio za magari Iringa, IMSC, pia imewataja wengin waliorudi ni Altaf Munge na Shahzadi Munge pia kutoka Dar es Salaam.

Orodha ya washiriki iliyowekwa hadharani na mwenyekiti wa IMSC, Robert Maneno, pia imemtaja Mtanzania aishiye Uganda, Yassin Nasser anatarajia kuwepo Iringa na mwaka 2023 ndiye alikuwa mshindi.

Waleed Nahdi na Samir Shanto watauwakilisha mkoa wa Morogoro wakati wenyeji wa mchezo ni Diwani Hamid Mbatta na Ahmed Huwel kutoka Iringa.

Maneno alisema mashindano yataanza rasmi tarehe 24 Mei katika Uwanja wa Samora katikati ya Mji wa Iringa na kumalizika tarehe 25 Mei katika  Shamba la Mt Huwel, nje kidogo ya mji wa Iringa.