Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota wapya Simba waikabili Gwambina FC

Muktasari:

Walioko benchi ni Ally Salum, Twaha Ayubu, Maulid Zumba na Geoffrey Samwel,Pascal Jophin na Mwinyi Ally.

WACHEZAJI wapya wa Simba, Kennedy Juma na Miraji Athumani ni miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha timu hiyo kinachocheza mechi ya kirafiki ya uzinduzi wa uwanja wa Gwambina uliopo wilayani Misungwi, jijini Mwanza.
Simba inacheza mechi hiyo na timu ya Gwambino FC ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo ambao umekusanya mashabiki wengi.
Simba imemsajili Juma akitokea Singida United na Miraji aliyekuwa akiichezea Lipuli FC msimu uliopita.
Katika kikosi cha simba mbali na wachezaji hao wengine ni Deogratius Munis 'Dida', Mzamiru Yasin, Emmanuel Kichiba, Yusuph Mlipili, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Ben Jacob , Menzi Thill na Rashid Juma.
Walioko benchi ni Ally Salum, Twaha Ayubu, Maulid Zumba na Geoffrey Samwel,Pascal Jophin na Mwinyi Ally.
Ikimbukwe kuwa Gwambina FC ndio iliyokuwa inaitwa Arusha United ambayo imeuzwa na wamiliki wake JKT Oljoro na imenunuliwa na mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti na kuihamishia nyumbani kwao Misungwi ambapo msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwakilisha Mwanza