Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Novatus akutana na Marseille

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ukraine kwenye  timu ya Shakhtar Donetsk, atakuwa na safari yakwenda nchini Ufaransa mwakani kwa ajili ya kucheza dhidi ya Marseille kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League.

Katika droo ya michuano hii ambayo imefanyika huko Nyoni nchini Uswiss, Shakhtar ambayo imeingia kwenye michuano hii baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, inakutana na Marseille ambayo haijawahi kuchukua kombe hili licha ya kucheza fainali mara tatu, mara yamwisho ikiwa ni mwaka 2018.

Kwa upande wa Shakhtar yenyewe inaonekana kuwa na historia nzuri zaidi kwenye michuano hii kwani imewahi kuchukua ubingwa msimu wa 2008-09.

Droo yote ni hii,
Shakhtar Donetsk v Marseille
Galatasaray v Sparta Prague
Braga v Qarabag
Benfica v Toulouse
Young Boys v Sporting
Lens v Freiburg
AC Milan v Rennes
Feyenoord v Roma